.....Ibada hiyo ilifanyika tarehe 11/01/ 2015 katika ukumbi wa MD 1 chuo kikuu Bugando..
......ilikua ni ibada ya kwanza kwa mwaka 2015 , ilibada ilifunguliwa kwa maombi...
....timu ya kusifu na kuabudu ilifuata kwa kuongoza sifa pamoja na kuabudu....
....kwaya ya USCF-Bugando nayo haikuwa nyuma, kwani nao walihudumu katika sehemu yao walioitiwa na Bwana kuhudumu...
....somo la kwanza lilitoka Zaburi 1:1-6, na somo la pili lilitoka Yohana 15:1-4...
....katibu mkuu wa USCF-Bugando aliweza kutoa matangazo ya usharika......washarika nao walimuimbia Muumba wao kwa Tenzi za Rohoni...
...hatimaye ulifika wakati wa mahubiri, ambapo Mtumishi wa Mungu aliyetumwa kuja kusema na kanisa kwa siku hiyo alikuwa ni Mama Kitulo.
-Mhubiri 12:1 -ndio mstari uliokuwa wa kwanza akihimiza kumkumbuka Muumba wetu katika siku za ujana wetu...
..pia aliweza kuzungumzia juu ya uthamani wa sadaka Mwanzo 4:3-6.
...mwisho alisemea umuhimu wa kuweka malengo ya mwaka kama Wakristo
Mithali 16:1-3,9 Mithali 8:17-21, Mithali 3:5-6
Zaburi 32:8 Zaburi 50:5,14-15 Zaburi37:3-4
.....maombi maalumu ya kufungua mwaka yaliongozwa na mratibu wa maombi wa USCF....
.....washarika walimtolea Mungu sadaka na Shukrani zao kwa mambo makuu aliyowatendea....
....mwenyekiti alitoa zawadi kwa wale washindi wa bonanza lilifonyika chuoni SAUT.....
....katibu aliwezesha changizo la kununua kamera ya USCF na kiukweli washarika walijitoa sana na MUNGU wetu wa mbinguni awabariki
......Ibada ilihairishwa kwa maombi...
TAFAKARI YA LEO: JE, MWAKA HUU UNAMALENGO GANI?..
SHUKURANI ZETU KWA MHUBIRI -MAMA KITULO,
MUONGOZA IBADA-KAKA AGRIPA ELIREHEMA (MD 5)
UONGOZI WA CHUO CHA BUGANDO
UONGOZI WA USCF TAWI BUGANDO
MAFUNDI MITAMBO
KWAYA YA USCF-BUGANDO
TIMU YA KUSIFU NA KUABUDU BUGANDO
NA WASHARIKA WOTE WALIOOMBEA NA KUSHIRIKI KWA NAMNA MBALIMBALI KATIKA IBADA HIYO
....MUNGU WETU TUNAYEMTUMIKIA AWABARIKI WOTE NA KUWATIA NGUVU KATIKA KAZI YAKE...
...AMEN..
No comments:
Post a Comment