NGUVU ILIYOSITIRIKA NDANI YA KUSOMA VITABU BY PASTOR; JAMES KALEKWA

Utangulizi
Kitu kinachoamua kiwango cha uhuru kwenye maisha yako ni kiwango cha ufahamu ulichonacho
Kiwango cha kutokuwepo kwa giza kinaamuliwa na kiwango cha uwepo wa mwanga (Mwanga unapokuwepo kwa wingi zaidi basi giza huwepo kidogo zaidi)

Uko jinsi ulivyo kwasababu ya kiwango cha ufahamu – Ukiongeza ufahamu, utajiongezea uhuru!

Maandiko:
Yohana 8:32

Mifano:
Allegory of the Cave by Plato
Kufikiri jambo usilolijua
Kusoma vitabu ni moja ya njia (njia kubwa sana) ya kuongeza uhuru kwenye maisha yako

Mwanaharakati # 1. Danieli
Rejea Danieli 9:1-3 Kwa kuvisoma vitabu(Greek: Biblia= books)
(Yer 25:11-12; 29:10; 30:18; 2Nyakati 36:21)
ü Alikuwa na miaka 15  wakati wa utumwa
üAlikuwa mshauri wa wafalme wanne/awamu nne
          605 K.K Taifa lilichukuliwa utumwani 
          538 KK Ufunuo/Uamsho ndani ya moyo wa Danieli (mwaka wa 67) na mwaka wa 68 taifa lilipokea uhuru.
Kimsingi, taifa lilipaswa kukaa utumwani miaka 70 = kusoma vitabu kuliharakisha uhuru.
Utimilifu wa harakati: Ezra 1:1-6

Mwanaharakati # 2. Musa
Rejea Kutoka 2:11-15
(Mwanzo 15:12-14)
Misimu:
Utumwa & Mateso: miaka 400 ya hali ya ukiwa katika nchi ya ugeni
Uhuru & Mafanikio – kipindi cha utoshelevu:
Rejea
MDO 7:22-30; Kut 12:40-41
Utumwa wa Israeli (Misri) ulidumu kwa muda mrefu kwasababu haukuwa na hamasa ya vitabu (was not book inspired)

Mwalimu Nyerere na Uhuru wa Tanganyika
Baada ya vita kuu za dunia (WW I&II), nchi ya Ujerumani ilipoteza sehemu kubwa ya makoloni.
Umoja wa mataifa uliiweka Tanganyika mikononi mwa Uingereza kwa uangalizi
Tanganyika ilipaswa kujiandaa kujitawala na wakati ilipokuwa tayari ilipaswa kuomba uhuru wake
Masharti hayo ya Umoja wa Mataifa kwa  Uingereza yalikuwa kwenye mfumo wa maandishi
Ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye alipata fursa ya kusoma na kuongoza harakati za uhuru

Hitimisho:
Msingi wa Tanganyika umo kwenye usomaji wa vitabu = Tanganyika ilijengwa kwa kusoma vitabu, itatunzwa kwa kusoma vitabu!

                                                 PASTOR; JAMES KALEKWA

No comments: