..ibada ilifunguliwa kwa maombi ikifuatiwa na timu ya kusifu na kuabudu ya Bugando ambayo pia ilitoa huduma ya kusifu na kuabudu.....
![]() |
muongoza ibada DR. Marko Hingi |
![]() |
timu ya kusifu na kuabudu |
....kwaya ya Bugando pia ilihudumu ikifuatiwa na waimbaji binafsi....
![]() |
mwimbaji binafsi wa USCF |
...katibu wa USCF alitoa matangazo ya usharika...
.....wanaUSCF Bugando walipata neema ya kulishwa neno la MUNGU na mtumish wa MUNGU Mch. Raymond kutoka Redio maarufu jijini Mwanza ijulikanayo kwa jina la Kwaneema Fm....
UJUMBE: Usikubali kukata tamaa au kukatishwa tamaa ya maisha.
-Daudi alikatishwa tamaa na ndugu zake kuwa hawezi kumshinda Goliath, lakini aliweza kushinda,..
-Yusuph pia aliuzwa na ndugu zake, alitupwa gerezani kwa kesi isiyo ya kwake, lakini hakukata tamaa na mwisho alitimiza ndoto yake..
MASOMO: 1 Samwel 17, Daudi 17:17
- Mengi yalisemwa ikiwemo pamoja na kutojidharau kuona hatufai mbele za Mungu aliye juu
![]() |
Mch. Raymond akitoa huduma |
![]() |
Mch Raymond akitoa huduma |
...Mtumishi aliweka wakfu kamera mpya iliyonunuliwa kupitia mkono wa wanaUSCF kwa neema ya Mungu. kamera hiyo ni aina ya Fujifilm SL 300.....
....Shukurani na sadaka za kawaida zilifuata, wakati ibada ikipambwa moto na mwimbaji binafsi, pamoja na dada Asha (MD 5)...
....maombi ya wanaUSCF wote yakiongozwa na mratibu wa maombi yalifuata na mwisho ibada ilihairishwa kwa maombi na kwaya ya USCF wakamalizia....
TAFAKARI YA LEO: JE, WEWE UNATHAMANI GANI MBELE ZA MUNGU...?..
UJUMBE: MUNGU HAANGALII KAMA WANADAMU WAANGALIAVYO
MUNGU HUVIINUA VINYONGE NA KUVIFANYA KUWA NA NGUVU
SHUKURANI ZETU : MUNGU WETU PAMOJA NA JESHI LA MBINGUNI
MUONGOZA IBADA- MARKO HINGI (MD 5)
MUHUBIRI- MCH.RAYMOND
KWAYA YA USCF BUGANDO
TIMU YA KUSIFU NA KUABUDU BUGANDO
DPS 2 NA KAMATI NZIMA YA MAPAMBO
VIONGOZI WA USCF BUGANDO
WANAUSCF WOTE
UONGOZI WA CHUO NA HOSPITAL BUGANDO
WOTE WALIOHUSIKA KATIKA IBADA HIYO
NYOTE MBARIKIWE NA MUNGU ALIYE HAI
.....Shalom..
...USCF-Bugando (UKWATA) inayo furaha kukukaribisha katika ibada ya kumtukuza Mungu..
...mahali ni chumba cha MD1, ....
..ni jumapili ya tarehe 18 /01 /2015...
....fika bila kukosa na ubarikiwe...
IBADA ILIYOFANYIKIA ST.NICOLAS ANGLIKANA 13/05/2012
Tumepewa ujumbe ambao ni KUUSHINDA ULIMWENGU
1Yohana5:1-12
Yohana16:16
Mtumishi wa Mungu alisema: Watu wa siku hizi hawajui jinsi ya kuushinda ulimwengu
wanazani kuushinda ulimwengu ni kuwa tajiri (kufanyikiwa kimaisha).
Kuushinda ulimwengu ni kushinda majaribu kama jinsi mtumishi wa Mungu Ayubu kwani yeye aliushinda ulimwengu kwa jinsi ambavyo majaribu mengi yaliyo mpata lakini Ayubu aliweza kuyashinda.
Nikiwa na Mwana (Yesu kristo) najua kuwa nina uzima kwani hakuna kitu ambacho kitakatisha maisha yangu
Mtumishi wa Mungu pia akasema: Watu wakiwa na Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI) ndipo unaona watu wanahangaika kutafuta kinga,kutafuta dawa za kuongeza kinga mwilini.
Lakini watu wakiwa na Upungufu wa kinga Rohoni(UKIRO) hawahangaiki kutafuta kinga rohoni,kinga ya Roho ni Yesu kristo hivyo imetupasa kumtafuta Bwana Yesu.
MUNGU ATUSAIDIE ILI TUWEZE KUUSHINDA ULIMWENGU
Asiye na Yesu kristo hawezi kuushinda ulimwengu.
.
IBADA YA PAMOJA YA UKWATA ILIYOFANYIKA TAREHE 06/05/2012
Tunammshukuru Mungu kwaajili ya uwepo wake ndani ya ibada ni mengi ambayo Mungu amesema nasi kupitia ibada iliyofanyikia Chuoni kwetu.
Amesema nasi kwanjia ya uimbaji pia mahubiri kwa njia ya neno kupitia kinywa cha mtumishi wake
Somo ambalo Roho Mtakatifu ametufundisha ni KANUNI NA SIFA ZA KUWA MFUASI WA KRISTO:1Kor 4:5,Luka 12:42,2Timotheo2:15,Isaya 41:8,Isaya 45:1
Kanuni na sifa hizo ni 1:KUWA MTUMWA WA KRISTO
2:KUWA WAKILI WA KRISTO
Ukiwa na sifa hizo utatambua dhamana uliyo pewa na Mungu.
Mungu amekuchagua ili umtumikie kama jinsi Yakobo alivyo chaguliwa kutoka katika uzao wa Ibrahimu ndani ya Taifa la Israel(Isaya 41:8)
Lakini pia Yesu anatuuliza swali anasema NI NANI ALIYE WAKILI MWAMINIFU MWENYE BUSARA AMBAYE BWANA WAKE ATAMWEKA JUU YA UTUMISHI WAKE WOTE AWAPE WATU POSHO KWA WAKATI WAKE?.
Kwaya ambazo ziliihudumu katika ibada ni UPENDO KWAYA kutoka K.K.K.T-BUGANDO
pia na WANA HAUTIKISIKI CCT-UKWATA BUGANDO
SHUKRANI UONGOZI WA UKWATA UNATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WANAUKWATA WOTE,KWAYA ZILIZO HUDHURIA,WAGENI WAALIKWA NA WANAFUNZI WOTE KWA USHIRIKIANO MKUBWA KATIKA KUFANIKISHA UZINDUZI ULIOFANYIKA TAREHE 01/07/2012.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE KWANI AMETUTENDEA MAMBO MAKUBWA SIKU YA UZINDUZI HUWEZI KUELEZEA.
KILA MTU ALIYEHUDHURIA SIKU HIYO ALIBAKI AKIMSHANGAA MUNGU.
ENEO LA PARKING AREA LILIJAZA WATU KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWANZA.
CCT-UKWATA BUGANDO CHOIR MTALIPWA NA MUNGU MAANA TABU YENU WALA SI BURE.
SHEREHE YA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA 2012/2013
Uongozi wa ukwata unawashukuru wanaukwata kwa ushirikiano mliouonyesha katika
kufanikisha sherehe ya kuwa karibisha wanaukwata wenzetu wa mwaka wa kwanza 2012/2013
Mungu awabariki wanaukwata wote,Kwaya ya AICT-BUGANDO,PRAYS& WORSHIP TEAM
na CCT-UKWATA BUGANDO KWAYA(WANA HAUTIKISIKI)

No comments:
Post a Comment