HALELUYA; BWANA YESU ASIFIWE ,
Kwa mapenzi yake mola ibada hiyo ilikuwa ya kubarikiwa sana kwa wanaukwata na wakristo wengine wote walohudhuria. Matawi ya UKWATA yaliyohudhuria yalikuwa matano yaani BUGANDO,VETA,FISHERIES,MIPANGO-BWIRU na BUTIMBA.
Pia ibada hiyo ilikuwa na kwaya zilizotoa mahubiri kwa njia ya nyimbo zenye kumsifu Mungu na kwaya hizo ni CCT KWAYA BUGANDO, BUTIMBA KWAYA, WISDOM BAND na JERUSALEM BAND.
Mchungaji SEVERINE KISENGE alihudhuria pia ibada hiyo na aliyewalisha neno la Mungu siku ya ibada hiyo alikuwa mtumishi wa Mungu Mwalimu JAKOBO alihubiri sana juu ya UMOJA na WOKOVU kwa kusema kuwa sote tu madhehebu mbalimbali lakini tunamtumikia YESU KRISTO PEKEE na si binadamu kwa hiyo tunapaswa kumtumikia kwa umoja pia tunapaswa kumtumikia YESU KRISTO kwa unyenyekevu zaidi na tunapaswa kuwa na wokovu, na masomo yalipatikana katika ZABURI 133:1 , MITHALI 18:1, 1WAKORITHO 1:10 -13 , MARKO 7:21 - 23 na YEREMIA 32:40
Mtumishi wa bwana Mwalimu JAKOBO akihubiri neno la Mungu.
JERUSALEM BAND WAKITOA BURUDANI.
WARATIBU MBALIMBALI WA UMOJA WA VYUO UKWATA MWANZA.
JERUSALEM BAND.
Mch. SEVERINE KISENGE akitoa maelekezo mbalimbali.
WENYEVITI WA VYUO MBALIMBALI WA MATAWI YA UKWATA.
WANAKWAYA WA UKWATA - BUTIMBA
No comments:
Post a Comment