Mafundisho / shuhuda /mahubiri



Ufunuo Wa Yohana 21:27

Watoto wa MUNGU nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI ambaye lengo lake yeye kuja ulimwenguni ni kututoa katika njia ya jehanamu na tumfuate yeye katika njia ya mbinguni. Nitaelezea kuhusu njia ya jehanamu uijue nitaelezea kimwili pia na kiroho. Njia hii ya jehanamu kiongozi wake ni yesu kristo wa uongo anaitwa wa uongo sababu ili amteke mtu silaha yake kubwa ni kumpa mwanadamu elimu ya uongo kwa kulibadilisha neno la MUNGU, na kuvunja amri za MUNGU.

1.     KIMWILI

Njia hii ya jehanamu kwanza kabisa ni pale unapoona mtu anatenda dhambi, anapoyatenda hayo yafuatayo nitaelezea haijalishi ameokoka au yeye ni mkristo hewa.
Kufanya uzinzi, ulevi, kuabudu sanamu, kuwa na wivu, chuki, kuvuta bhangi, sigara, madawa ya kulevya, kwenda disko, kucheza na kuimbe miziki ya kidunia, kusema uongo, kuoa wake zaidi ya mmoja, uwizi na matendo yote ya ufisadi (endapo unayefanya hayo uelewe upo katika njia ya jehanamu siyo ya mbinguni haijalishi unasema unaenda mbinguni) je hayo unayofanya ni matendo ya mbinguni? Jibu siyo.

2.     KIROHO

Haya nitakayoyataja ni baadhi tu ambayo yatakupa picha ujielewe katika roho je upo salama au tayari kiroho upo jehanamu na umeishikilia njia yake kwenda motoni. Kwanza kabisa hakikisha kuhani wako ni kweli MUNGU ndiye kamleta, kama amejiita au ni mchungaji wa mshara uelewe roho zenu zinapelekwa katika njia pana ya jehanamu katika ulimwengu wa roho , kuabudu sanamu, misalaba, ibada za wafu, ubatizo wa kikombe, maji ya kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji, kubatizwa ukiwa mtoto mdogo, kushiriki katika kanisa lolote lile ambalo linachangisha pesa kanisani au mahali popote pale, imeandikwa nyumba ya MUNGU ni nyumba ya sala, sasa ikiwa ni kinyume elewa hapo siyo mahali pa njia ya mbinguni, hapo ni mahali pa njia ya jehanamu katika ulimwengu wa roho, na uelewe pia ili uende mbinguni ni lazima katika uliwmengu wa roho uyafuate yale ya kweli tu katika biblia na siyo kinyume au kuchanganya uongo na ukweli hapana.

Kanisa lenye huduma sita zadala ya zile tano tu alizozianzisha YESU hapo pana njia ya jehanamu, huduma hii ya sita inaitwa Askofu, ukiona kiongozi wa kanisa amevaa kofia akihubiri ujue anawapeleka watu katika njia ya jehanamu. Zaidi soma makala ya Nabii Hebron Tanzania, nimeelezea mengi alivyonifundisha YESU ili niwafungue watoto wake macho na fahamu zao wapone roho zao sababu wengi mno wanapotezwa badala ya kuwekwa katika njia ya mbinguni sasa katika ulimwengu wa roho wameishika njia ya jehanamu. Japo na waumini hawapendi kwenda jehanamu, wanaongozwa na viongozi vipofu kiroho na kuwafanya waumini nao wawe vipofu wasimuone MUNGU wala kufika mbinguni. Ukiongozwa na mtumishi yeyote ambaye jina lake lipo kwenye mtandao wa freemason Internet au ni mchawi au mfanya mazingaumbwe, mfufua misukule au yeye mwenyewe hajabatizwa ubatizo ulioko katika katiba ya MUNGU yaani biblia, au anayeongozwa na nguvu za mizimu au anayejiita yeye ni YESU au kujifananisha na MUNGU au anajiita mungu mtu au mzinzi, mlevi, anachangisha watu pesa, hawa wote wanawapeleka watu jehanamu hayo ni matendo ya shetani na biblia imekataa. Au mtumishi yeyote aliyeitwa na YESU halafu akamsaliti hapo elewa hakuna tena njia ya mbinguni, ndani yake ni yesu wa uongo amekaa hivyo yesu huyo wa uongo atawaongoza watu katika elimu ya uongo ili awadumaze roho zenu na mpofuke msione njia ya mbinguni bali mbakie katika njia ya jehanamu na ile siku ya mwisho watu watalia na kusaga meno sababu watavuna wasichotegemea badala ya paradise ni jehanamu.

Mwana wa MUNGU ulilopo katika taifa lolote simama imara leo hii hali ni mbaya huu ni wakati wa hatari, kufumba macho na kufumbua ipo siku utakuta wengine wamenyakuliwa katika unyakuo na wengine walio katika njia ya jehanamu kimwili na kiroho watabakia hapo hapo wateseke kwa muda wa miaka saba na mpinga kristo, kataa sasa mafundisho ya mpinga kristo ili usije ukabakia hapa ulimwenguni wakati wa unyakuo, watakaobakia ni wale wapinga kristo (changanya neno na uongo) na watenda dhambi, na kila mtu ambaye hajaokoka na kuzaliwa mara ya pili. Zaidi uwatumie na wengine ujumbe huu ili wasome na wafunguke na wewe utabarikiwa na YESU WA NAZARETI.

NOTE:

BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote naomba leo uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele unitoe katika kitabu cha njia ya jehanamu, uniongoze wewe YESU na ROHO MTAKATIFU peke yake nyie ndio kweli, shetani sikutaki na mpinga kristo sikutaki katika jina la YESU WA NAZARETI aliye hai.

NABII HEBRON.

....****MWISHO****....





ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO
Na: Patrick Sanga
Salaam katika jina lake BWANA Yesu,
Katika Waefeso 1:17 Biblia inasema ‘Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE’.
 Hili moja ya maombi muhimu ambayo Mtume Paulo alifanya kwa jili ya Kanisa la Efeso. Kila nisomapo mstari huu nimekuwa nikijuliza sana ni kwa nini Mtume Paulo aliomba maombi haya kwa kanisa hili?.

Katika kutafakari na kuendelea kujifunza niligundua kwamba kulikuwa na sababu kubwa tatu ambazo zilimpelekea Mtume Paulo kuwaombea jambo hili, na kutokana na umuhimu wake hata kwa kanisa la sasa ndiyo maana nimeona ni vema nikaliandika hapa ili na wewe msomaji uweze kujifunza.

Zifuatazo ni sababu kadhaa zilizompelekea Mtume Paulo aliombee kanisa la Efeso roho ya hekima na ufunuo na kwa sababu hiyo zinatusaidia kujua umuhimu wake kwa kanisa la sasa pia;
Ili waweze kumjua Mungu zaidi (Waefeso 1:17)
Waefeso 1:11 ‘Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake’.

Kazi ya roho ya ufunuo ni kumfunua Mungu kwa kiwango ambacho bado hujakiona wala kukizoea ili kuboresha uhusiano wako na Mungu na kukufanya umaanishe katika kumpenda. Ndiyo, lengo ni kumfunua Mungu kwako, kutoka kwenye kona tofauti tofauti ili umjue zaidi ili hali kazi ya roho ya hekima ni kukupa ufahamu (maarifa), werevu na busara katika kufanya maamuzi sahihi kuhusu uhusiano wako na Mungu na maisha yako kwa ujumla. Katika ufunuo kuna mambo ambayo Mungu atayaleta kwako na yanahitaji hekima katika kuyafasiri, kuyanena na kutenda.

Naam bado hatumjui Mungu kwa kiwango kitupasacho kumjua na ndio maana tunahitaji roho ya ufunuo. Roho ya ufunuo inamuongoza mtu kujenga mahusaino binafsi na Mungu wake tokana na ufunuo aliopata.  Roho hii inatuleta kwenye ufahamu muhimu kuhusu ulimwengu wa roho na kwamba ni lazima tuanze kuishi maisha katika ulimwengu wa roho kuliko vile tunavyoishi katika ulimwengu wa mwili ili kumjua Mungu zaidi.

Ili kujua mambo ambayo Mungu amewaandalia (1Wakorinto 2:9-10)
Katika fungu hilo Biblia inasema hivi ‘Lakini, kama ilivyoandikwa, MAMBO AMBAYO JICHO HALIKUYAONA WALA SIKIO HALIKUYASIKIA, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. LAKINI MUNGU AMETUFUNULIA SISI KWA ROHO. Maana Roho huchunguza yote, hata MAFUMBO ya Mungu’. Pia katika Waefeso 1:18 imeandikwa ‘MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU MJUE tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo’
Mungu anataka watu wake wajue kwamba yeye anayo mawazo (Yeremia 29:11), mbalimbali ambayo amewaandalia watoto wake. Mawazo hayo yameunganishwa na kusudi la kuwepo kwao hapa duniani na hawana budi kuyajua, kuyapata na kuyatenda. Naam ili wafikie hapo sharti juu yao na ndani yao, wawe na roho ya hekima na ufunuo.
Kumbuka katika kila nyanja ya maisha iwe kazi, uchumi, biashara, familia, huduma, ndoa nk, yapo mambo ambayo ameyaandaa na anataka uyajue. Naam ni jukumu lako kuendelea kujenga na kuboresha mahusaino yako na Roho Mtakatifu yawe mazuri daima.

Ili kuujenga mwili wa Kristo ipasavyo
Katika 1Wakorinto 12:7 Biblia inasema ‘Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana’.  Ukiendelea Katika 1Wakorinto 12:20 imeandikwa ‘Na jicho haliwezi kuuambia mkono, sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuaimbia miguu; sina haja na ninyi’ na ule mstari wa 25 unasema ‘Ili kusiwe na faraka katika mwili, BALI VIUNGO VITUNZANE KILA KIUNGO NA MWENZIWE(1Wakorinto 12:25).

Hivyo roho ya ufunuo inatoa ufunuo ili kufaidiana, lengo ikiwa ni kuusaidia mwili wa Kristo kuimarika zaidi. Naam kumbuka ufunuo huu ni kwa sehemu kwa lengo la kulijenga kanisa, mwili wa Kristo. Katika 1Wakorinto 12:11 imeandikwa ‘Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye’. Na tena Mtume Paulo anamalizia kwa kusema ‘Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake’ (1Wakorinto 12:27).

Naam hakuna mtu anayepewa karama zote, kila mmoja anapewa kwa SEHEMU kama KIUNGO ili kwa kushirikiana, MWILI wa Kristo ujengwe vema. Naam kila kiuingo lazima kihakikishe kina kuwa na ufanisi unaotakiwa, si kwa ajii yake, bali kuhakikisha mwili wa Kristo unajengwa ipasavyo, kupitia ufunuo/uwepo wa kile kiungo.

Kanisa lazima lifike mahali pa kuwa na uelewa kamili juu ya mwili wa Kristo unavyopaswa kutenda kazi kupitia ufunuo wa Roho Mtakatifu kwa kuwa ‘Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka (1Wakorinto 12:18). Naam kila mshirika unayemuona NI KIUNGO CHA MWILI WA KRISTO KUPITA KARAMA, VIPAWA NA HUDUMA ALIZOPEWA kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo.  Roho ya hekima ikuongoze kutenda na kujua kwamba karama, huduma na vipawa ulivyonavyo ni kwa ajili ya kuujenga mwili wa kristo.

Naam hatupaswi kumdharau mtu yoyote kutokana na hali yake ya nje kwa jinsi ya kibinadamu maana yeye ni kiungo kinachostahili heshima zaidi (1 Wakorinto 12:22) Kazi ya Mchungaji na viongozi wa kanisa ni kufuatilia ili kujua Mungu ameweka/ametoa/amefunua kitu gani (karama/vipawa/huduma) juu ya wale wanaowaongoza ili kuviendeleza kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo.

Hivyo kutokana na umuhimu wa roho ya hekima na ufunuo juu ya kanisa la Mungu na kwa mtu mmoja mmoja ni vizuri tukachukua au ukachukua hatua ya kuanza kumomba Mungu akujalie roho ya hekima na ufunuo wewe binafsi, familia yako, jamaa zako na kanisa kwa ujumla ili manufaa yake yawe dhahiri katika mwili wa Kristo ulimwenguni kote.

Roho ya hekima na ufunuo na iwe nanyi
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA!

....****MWISHO****....





MAMBO YA KUFANYA/KUZINGATIA KATIKA KIPINDI CHA UCHUMBA


Mpenzi msomaji tunakusalimu kwa jina la Yesu!

Baada ya kuwa tumepata maombi ya vijana wengi kutaka kujifunza habari za Uchumba, mke wangu pamoja nami tumeona ni vema tukaandaa somo hili ambalo tunaamini litafanyika msaada kwa vijana wengi ambao wapo kwenye uchumba au wanajiaandaa kuingia katika eneo hili. Hata hivyo somo hili ni pana sana, kwa sasa tumeandika vitu vichache vya msingi, tunaamini kwamba huko mbele tutaandika kitabu chake rasmi.

Katika kitabu cha Muhubiri 3:1 Biblia inasema “Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”. Hivyo mwanadamu katika maisha yake hapa chini ya jua  kuna vipindi mbalimbali anavyovipitia hii ni pamoja na kipindi cha uchumba kwa sehemu kubwa ya watu.   
Katika kipindi hiki yapo mambo mengi ambayo wachumba hufanya, mengine ni mazuri na mengine hayafai kabisa. Na hii yote inatokana hasa na mitazamo au tafsiri ya uchumba kwa watu husika. Fahamu kwamba tafsiri unayokuwa nayo juu ya mchumba wako ndiyo inayokuongoza kujenga mahusiano ya aina fulani pamoja naye.

Lengo la somo hili ni;
Kuongeza ufahamu wa wachumba kuhusu kipindi hiki na Kuwapa vijana maarifa ya kuwasaidia kuishi kwa nidhamu ya Ki-Mungu katika uchumba wao. Pia ni kuwafikirisha vijana wanaotarajia kupita katika kipindi hiki mambo ya kuzingatia. Si wachumba wengi wanajua, Mungu anawataka wafanye nini katika uchumba wao au kwa lugha nyingine si wachumba wote wanaojua kwa nini kipindi cha uchumba kipo. Naam katika somo hili tumeandika mambo hayo kinaga ubaga.
Kwa kuwa suala la uchumba ni pana na lina mitazamo mingi, yafuatayo ni mambo tuliyozingatia katika uandishi wa somo hili;
  • Kuna makundi mbalimbali ambayo yana taratibu zao kuhusu mchakato wa mtu kumpata mke au mume kikiwepo kipindi cha uchumba. Makundi hayo ni pamoja na makanisa, makabila, familia nk.
  • Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia.
  • Kuna baadhi ya wachumba hadi kufikia muda wanakubaliana kwamba watakuja kuishi pamoja walishafahamiana tangu zamani na wengine hawakufahamiana.
  • Wachumba wanaweza wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.
Lengo letu ni kuandika juu ya mwongozo wa Neno la Mungu katika kipindi cha uchumba. kwa lugha nyingine, je Mungu anataka wachumba wafanye nini katika kipindi chao cha uchumba?. Kumbuka uchumba ni kipindi/wakati. Basi kama ni wakati jua kabisa kuna baadhi ya mambo ambayo ni lazima yafanyike, kwani Biblia inasema katika Mhubiri 8:5b “ Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu”, neno hukumu linamaanisha maamuzi, mambo ya kufanya.
   
Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba;
Jambo la kwanza –  Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu
2Wakorinto 3:17 ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’.

Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya.

Kumbuka Paulo katika 2Wakorinto 12:9-10. —‘Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ….kwa hiyo napendezwa na udhaifu——- maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Hivyo Roho Mtakatifu atabadilisha tafsiri ndani yako za vyote unavyoona kwa mwenzako huenda juu ya umbile lake, umri wake, macho yake, kabila lake viwe vitu vya wewe kujivunia. Zaidi Roho Mtakatifu pia atakuongoza katika maombi yatakayosidia kuuondoa ule udhaifu ambao umekuja si katika mapenzi ya Mungu, yaani wa kishetani.
Jambo la pili – ni wakati wa kuweka msingi imara wa uchumba wenu na kufahamiana zaidi.

Hili jambo ni la muhimu  kuzingatia. Ni vema wachumba wakatafsiri na kuelewa vizuri maana ya uchumba. Wachumba wanapaswa kuwa na mipaka fulani katika uchumba wao na  kuwa makini kwa kujilinda na mazingira ya kila namna ambayo yanaweza yakapelekea wao kuanguka dhambini. Ni vema mkajua kwamba ninyi ni wachumba na si wanandoa. Na kama ni wachumba basi uchumba una mipaka yake na hamruhusiwi kufanya mambo ya wanandoa. Mipaka hii iwe kwa habari ya kutembeleana,kupeana zawadi, mawasiliano (ingawa mnapaswa kuwa makini na lugha mnazotumia pia) nk.  Lengo la kutafsiri misingi ya mahusiano yenu ni kujiwekea mipaka na mazingira yatakayowasaidia kuishi maisha ya nidhamu, ushuhuda na kumletea Mungu utukufu.

Sambamba na hili sehemu kubwa ya wachumba huwa wanakuwa hawafamiani vizuri. Japo wapo baadhi ambao walianza tangu shule za msingi/sekondari/chuo na sasa wamechumbiana hivyo kwa sehemu wanafahamiana vema. Kwa wale wasiofahamiana vema huu  ni wakati wa kumjua mwenzako vizuri kwa maana ya kabila lake, familia yake, umri wake, interest zake, matatizo aliyo nayo yeye binafsi au ya kifamilia, mitazamo yake juu ya mambo mbalimbali kama uchumba, ndoa, maisha, wokovu, neno la Mungu nk. Huu ni wakati wa kumjua mwenzako kwa njia ya maswali mbalimbali ya msingi yanayohusu vitu nilivyovitaja hapo juu. Lengo hapa ni kujua mapungufu/madhaifu(weakness) na mazuri(Strength) za mwenzako ili mjue namna ya kukabilana na mapungufu na namna ya kuendeleza yaliyo mazuri.

Ni vema pia kuulizana historia zenu za maisha ya nyuma. Kabla ya kuokoka umepitia katika mifumo gani ya maisha ambayo imechangia kukufanya uwe ulivyo. Kabla ya kumpata uliye mpata ulikuwa umefuatwa na wangapi na uliwakubalia au la, na kama uliwakubali kwa nini mliachana, na sasa wako wapi, je bado wanakufuatilia. Hii itawasaidia sana kujipanga vizuri kimaombi na katika mahusiano yenu na zaidi itawasaidia kuweza kuchukuliana na kuhifadhiana katika madhaifu ya kila mmoja.

Mungu anapowaunganisha anakuwa na kusudi maalum. Hivyo jua kwamba huyo mwenzi uliyepewa umepewa kwa ajili ya kusudi fulani la Mungu. Ni wachumba wachache sana ambao pindi wanapokutana kila mmoja anakuwa anajua walau kwa sehemu kwa nini aliumbwa. Sasa ni vema mkae chini mfikiri, nini Mungu anataka kukifanya duniani kupitia ninyi? Na zaidi angalieni kazi zenu au yale mnayoyasomea, Je mtawezaje kuliimarisha agano la Bwana kwa pamoja kama mke na mume?.

Hapa maana yetu mnatakiwa kujibu maswali yafuatayo? Je ni kwa nini mlizaliwa? Je kwa nini Mungu amekuunganisha na huyo uliye naye sasa? Na je kupitia elimu, bisahara zenu au kazi mlizonazo mtawezaje kuimarisha agano la Bwana?, Kwa kuzingatia vipawa na uwezo Mungu aliowapa, je ni wapi Mungu anataka kuwapeleka na kuwafikisha? Kama ndani yenu mna huduma fulani, je ni watu gani ambao Mungu atataka mshirikiane nao katika huduma hiyo?, je ipi ni nafasi yenu katika mwili wa Kristo na taifa kwa ujumla? Ni vema zaidi mwanaume akajua wito/ kusudi aliloitiwa ili pia amshirikishe na mwenzake.
Kufanikiwa kwa hili kunahitaji uwepo muda wa kutosha wa wachumba kukutana ili kupanga na kuweka mambo yao mbalimbali, na kama ni watu walioko mbali basi suala la mawasiliano kwa njia mbalimbali kama simu, barua pepe, na barua na hata zawadi ni la muhimu.

Jambo la tatu– ni wakati wa kulinda wazo la Mungu hadi litimie.
Siku zote uamuzi wowote unaoufanya una gharama. Naam uchumba pia una gharama nyingi Sana za kuzikabili kuliko unavyofikiri. Gharama hizo ni pamoja na muda, pesa, mawasiliano, maombi, uhuru nk. Kumpata mchumba au mwenzi ambaye ni wa kusudi la Mungu, usidhanie ndio umemaliza. Kama huo uchumba wenu ni wa mapenzi ya Mungu muwe na hakika mtakutana na vita kubwa sana katika kipindi hicho cha uchumba na lengo ni kuwatenganisha. Ni lazima mjifunze siku zote kuombeana kwa kumaanisha maana Shetani naye yupo kazini ili kuvuruga hayo mahusiano.

Kumbuka huyo mwenzi ni agano toka kwa Bwana hivyo unawajibika kumlinda, kumlinda ni pamoja na kuhakikisha wewe hausabibishi au haufanyiki chanzo cha ninyi wawili kuanguka dhambini, au ukamwacha na kumsababishia majeraha ya nafsini na hivyo kuharibu mahusiano yake na Mungu. Wapo watu waliofikia kuharibu mahusiano yao na Mungu kisa mchumba, saa ya ibada imefika mchumba anasema twende zetu out bwana, unataka kufanya maombi ya kufunga mchumba anasema kesho nitakutoa out, inagharimu sana muda wa kuwaza pia kwa ajili yake na familia yake au mahitaji mbalimbali aliyo nayo.
Zaidi pia uchumba unaweza kukunyima uhuru hata wa kuwa na maongezi na rafiki zako, maana kuna baadhi ya watu huwa hawataki kuona mchumba wake anaongea au kucheka na watu wengine, na pia kuna wengine ni wachumba lakini wamewekeana taratibu ngumu utafikiri wanandoa kabisa na ukweli zinawatesa ila kwa sababu hataki kumpoteza huyo mchumba wake inabidi avumilie.  Jambo tunalosisitiza hapa ni kwamba, uchumba una gharama nyingi angalia mahusiano yako na Mungu yasiharibikie hapa.
Jambo la nne– ni wakati wa kupanga malengo na mikakati yenu ya baadae.

Mithali 29:18a “Pasipo maono, watu huacha kujizuia’
Hili si jambo ambalo vijana wengi hulipa kipaumbele linavyostahili. Katika hili ni vema wachumba wafikirie mapema ni aina gani ya maisha ambayo wangependa kuwa nayo, na pia je ni aina gani ya ndoa wanataka kufunga, tatu je ni wapi wangependa kuja kuishi kwa maishayaoyote. Haya yatawasaidia wahusika kujipanga ndani na nje kukabiliana na yaliyo mbeleyao.Kamawanataka kufunga harusi kanisani basi maana yake wanahitaji kuwa na maandalizi mazuri kifedha, waweke katika muda kila wanalotaka kuelekea katika harusiyaoili iwasaidie kujiaadaa mapema. Malengo yoyote yale ambayo mtaweka basi hakikisheni yanatekelezeka, yanafikika, yanapimika na mnayapangia muda wa utekelezaji.

Mambo zaidi ya kuzingatia katika malengo yenu;

Katika hili ni vizuri wachumba waangalie nafasi yao kifedha imekaaje, na changamoto zinazowakabili wote kwa pamoja. Je hali yao kifedha inawaruhusu kuzikabili gharama za maandalizi ya ndoa kwa ujumla. Je hali ya kimaisha ya kijana wa kiume inamruhusu wakati wowote baada ya kuchumbia aweze kufunga harusi kama anataka. Je nafasi zao kielimu zikoje, je kama zinatofautiana ni kwa kiwango gani? Na je tofauti zao kiuchumi na kitaaluma zinaweza kuwa kikwazo kwao kuoana, au kwa wazazi wao nk. Na je baada ya kuwa wamegundua na kupima uwezo wao katika hayo mambo mawili, je wanaweza wakasaidianaje ili wafike mahali pazuri wote wawili.

Vijana wengi wa kiume huwa wanakosea sana hapa, wengi huwa wanasema sitaki kuchumbia/kuoa mpaka niwe nimesha jikamilisha kiuchumi, niwe angalau na maisha mazuri. Sisi hatushauri sana dhana hii, ukweli ni muhimu kwa kijana wa kiume akjikamilisha kwa yale mambo ya msingi. Lakini fahamu kwamba kuna wakati mwingine kuendelea kwako kiuchumi, au kuvuka kwako kimaisha ni rahisi zaidi pale unapokuwa na mchumba au ndoa yako. Tunasisitiza tena ni vema wachumba wakae chini na kufikiri ni kwa namna gani wataendelezana kiuchumi na kitaaluma. Angalizo, ni vema uwe na uhakika kweli huyo mtu ni wa mapenzi ya Mungu kwa maana ya kuwa ni wa kwako kweli, maana wapo wachumba ambao wamekuwa wakisaidiana mpaka kulipiana ada, kupeana mitaji, kununuliana nyumba, magari nk, halafu mwishowe mmoja anavunja maagano, maumivu yake ni makubwa sana
.
Jambo la tano – ni wakati wa matengenezo na kuzijenga nafsi zenu
Wachumba wengi huwa wanafichana mambo mengi sana wanapokuwa wachumba na matokeo yake hawayashughulikii mapema na hivyo yanakuja kuwaletea shida kwenye ndoa. Huenda kabla hujakubaliwa wewe tayari mwenzako alikuwa amesha wakubali vijana au mabinti wengine kwamba ataolewa nao au kuwaoa. Pia  kama ni msichana huenda ameshawahi kubakwa, au kutokana na masumbufu ya kupata mtu sahihi na wakati mwingine kuachika mara kwa mara imefika mahali huyo msichana akasema sitaki kuja tena kuolewa. Zaidi  huenda  mmoja wenu huko nyuma ameshawahi kufanya uasherati au zinaa kabla hamjachumbiana. Au kuna mwingine amekuwa akisumbuliwa na tatizo la harufu, kufanya tendo la ndoa na mapepo nk.
Haya yote na mengine mengi yanayofanana na haya yana athari kubwa sana kiroho na kimwili kwenu kama wachumba na wanandoa watarajiwa kama hayatashughulikiwa vema katika kipindi hiki cha uchumba. Licha ya kuwa na athari mambo hayo yamepelekea nafsi za watu au wachumba wengi kujeruhika. Nafsi inapojeruhiwa inaharibu ndani ya mtu mfumo wa kufanya maamuzi, mfumo wa utiifu kwa Mungu wake, mfumo wa kunia na kuhisi pia. Sasa mifumo hii inapoharibika inapelekea watu kufanya maamuzi ambayo yapo nje ya mapenzi ya Mungu kabisa. Nawajua baadhi yao ambao wameacha na wokovu, na, wengine wamekata tamaa ya kuolewa, wapo walioamua kuolewa na mataifa ilimradi ameolewa nk.

Hivyo basi tumieni wakati huu kufanya matengenezo na kujengana nafsi zenu kwa maana ya kuombeana sana, pili kwa kuongeza ufahamu wenu katika neno  la Kristo hasa maandiko yanayolenga uponyaji katika nafsi zenu, tatu kufuta na kufisha mapatano/maagano yote ambayo mmoja wenu aliyafanya huko nyuma na watu wengine na pia kufuta picha za kubakwa na kujenga ufahamu wa mtu aliyeathirika kisaikolojia kutokana na mambo kama hayo kwa njia ya Damu ya Yesu. Hatua hizi zitawasaidia kurejesha mifumo iliyoharibika na kuziruhusu nafsi zenu zifanye kazi kama inavyotakiwa. 

Jambo la sita – ni wakati wa kujua taratibu mbalimbali kuelekea kwenye ndoa

Tumeshasema, kila dhehebu au kabila wana taratibu zao kuhusu uchumba hadi ndoa. Hivyo ni vema wachumba, wakafuata taratibu ambazo zimewekwa na makanisa yao hasa zile ambazo zipo katika mapenzi ya Mungu. Lakini pia lazima tukubali kwamba kuna baadhi ya taratibu za makanisa, makabila na hata madhehebu ambazo nyingine zipo tu lakini hazitekelezeki na nyingine hazimpendezi Mungu.

Sasa ni vema wachumba wazijue hizo taratibu na wajue je wanaweza kuzitekeleza au la, na kama hawawezi wafikirie kabisa wanafanyeje. Mfano kuna baadhi ya makanisa ambayo hayaruhusu mtu wa kwao aoe au kuolewa na mtu wa nje ya dhehebu hilo. Sasa hii ina maana kama una mchumba wa aina hiyo jipange kujibu maswali ya wazee wa kanisa na Mchungaji vizuri. Na zaidi kuna baadhi ya makabila na familia hazitaki uoe au kuolewa na watu nje ya kabila lako, au aliyekuzidi umri kama wewe ni kijana wa kiume nk. Hivyo ni vema kuzijua hizo taratibu ili mjue mnajipangaje kukabiliana nazo. Ushauri wetu ni huu kama una uhakika huyo mtu ni wa kutoka kwa Mungu basi simamia la Bwana maana lipi jema, kumpendeza Mungu au wanadamu?. Kumbuka Mungu ndiye mwenye ratiba ya kila mmoja wetu.

Suala la  kukagua/kupima afya zenu kwa pamoja.

Kwa mazingira ya ulimwengu wa sasa suala la ukimwi limechukua sura mpya na kuleta mtafaruku ndani ya kanisa hasa kwa vijana wanochumbia kabla ya kupima afya zao. Siku hizi jambo hili limewafanya wachungaji kuomba sana kwa habari ya vijana ndani ya kanisa. Sasa kama mlikuwa hamjapima afya zenu mpaka mmechumbiana basi chukueni hatua mwende kupima. Ni vema wachumba wakapima mapema afya zao ili jambo hili lisije likawaletea shida baadaye, maana kwa sheria ya nchi yetu wachungaji hawaruhusiwi kufungisha ndoa kama mmoja wa wahusika ameathirika.

Upimaji wa afya zenu ni wa muhimu kwani, ndani ya makanisa kuna rekodi ya vijana wengi tu ambao wameshaathirika na huenda si kwa sababu ya zinaa, maana kwa mujibu wa watu wa afya njia za maambukizi ni nyingi. Kuna wengine wamezaliwa nao, kwa nia ya kuongezewa damu,kutumia vifaa kama nyembe, sindano nk. Hata hivyo swali la msingi inabaki kwamba je, liko tumaini kwa mtu aliyeathirika kuoa au kuolewa?
   
Tukueleze hivi, hakuna jambo gumu lolote la kumshinda Bwana, hii ni pamoja na ukimwi, kama Mungu alimfufua Lazaro, alitenganisha bahari ya Shamu na watu wakapita, kama Yesu alitembea juu ya maji, basi naomba ujue kwamba Ukimwi hauwezi kuzuia kusudi la Mungu hapa duniani kwa wale awapendao na kwa sababu hiyo tunasema hata kama mtu ana ukimwi na Mungu bado ana kazi naye hapa duniani, hakika atamponya huo ukimwi na atampa mke au mme.

Faida na lengo la kupima ni hili, hata kama majibu yatatoka mmoja ameathirika isiwe mwanzo wa ninyi kuachana. Kama mna uhakika Mungu aliwaanganisha huu ndio wakati wa kurudi mbele za Mungu kwa maombi ya uponyaji na kujipanga zaidi juu ya hilo. 

Jambo la saba – ni wakati wa kuongeza ufahamu wenu kuhusu nafasi yako kwenye ndoa.

Je umeshawahi kujiuliza ni kwa nini Mungu anakupa mke au mme? Yamkini zipo sababu nyingi lakini baadhi yake ni; Mungu anakupa mke kama msaidizi, mlinzi, na pia unapopata mke au mme unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana na pia ni kwa sababu ya zinaa ndio maana unahitaji mwenzi. Hizi ni baadhi ya sababu zilizoko ndani ya Biblia. Hivyo basi tafuteni wanandoa mnaowaamini na zaidi waliokoka  muwaulize   kuhusu wajibu  wa kila mmoja kwa nafasi yake kwenye ndoa. Katika hili baadhi ya makanisa  huwa yana utaratibu wake wa nani atahusika na maelekezo ya aina hii kwa wachumba. Hivyo kama kanisa lako lina utaratibu huo, fuata huo utaratibu.

Katika ndoa kuna mambo mengi sana ambayo mtatakiwa kufanya, ni vema kufuata mwongozo na ushauri wa viongozi wenu au wachungaji wenu kuhusu nini mnatakiwa kufanya katika ndoa yenu. Angalizo hapa ni hili, uwe makini na vyanzo vya ushauri au mafunzo katika eneo hili ili lisije kuleta madhara baadae. Usitafute wala kufuata kila ushauri, bali sikiliza pia uongozi wa Mungu ndani yako.

Jambo la nane– Msifanye tendo la ndoa, maana jambo hili litaharibu mpango wa Mungu na kusudi lake kupitia ninyi.

Wakati wa uchumba, si wa kufanya mapenzi au kufanya michezo ya mapenzi. Tunarudia tena ili kuonyesha msisitizo kwamba chonde chonde jamani, uchumba sio ndoa, maana uchumba unaweza kuvunjika. Hairusiwi kabisa kwa wachumba kufanya mapenzi kwa maana ya tendo la ndoa kabla ya ndoa. Kitendo cha Mungu kukujulisha/kukupa huyo mwenzako kama mke/mume mtarajiwa haina maana mna haki ya kufanya mambo ya wanandoa. Mungu kukupa huyo mwenzako sasa ni taarifa kwamba  huyu ndugu ndiyo atakuwa mkeo au mmeo na anakupa taarifa sasa ili ujipange kufanya mambo ya msingi mnayotakiwa kuyafanya katika kipindi cha uchumba. Kipindi cha uchumba ndicho kipindi ambacho wachumba wengi sana wanavuruga kusudi la Mungu, na kuharibu maisha yao ya baadae na ndoa yao kwa ujumla.

Ndoa nyingi sasa hivi zina migogoro kwa sababu wakati wa uchumba walidiriki kufanya tendo la ndoa. Vijana wengi hawajajua kufanya tendo la ndoa kipindi cha uchumba lina madhara gani kwao na ndio maana wengine wanafanya. Biblia inasema katika Mithali 6:32 “Aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake mwenyewe”. Hata kama ukifanya tendo la ndoa na mchumba wako ambaye mlibakiza siku moja kufunga harusi, bado umezini.

Ndani ya nafsi ya mtu kuna akili, hisia, nia na maamuzi. Biblia inaposema afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake ana maana hii, dhambi hii inapofanywa, ina haribu mfumo wa utiifu na uamnifu kwa Mungu wako, inapelekea kukosa usikivu wa rohoni kabisa, ina haribu mfumo wa kufikiri, kunia na kufanya maamuzi. Na kwa sababu hiyo si rahisi tena kusikia na kutii uongozi wa Roho Mtakatifu. Kwa watu ambao wamezoea kuwa na mahusiano mazuri  na Mungu watanielewa ninachosema hapa.

Zaidi kuna baadhi ya wachumba kweli hawafanyi tendo la ndoa bali wanafanya michezo ya mapenzi. Michezo ya mapenzi (Fore play) ni maalum kwa ajili ya wanandoa, na ni sehemu ya tendo la ndoa. Hivyo kufanya michezo ya mapenzi ni kufanya mapenzi kwa sababu ile ni sehemu ya mapenzi. Kuna vitu unavichochea,  unaamusha hamu ya mapenzi au unayachochea mapenzi. Biblia inasema katika Mhubiri 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala  wa porini, msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vema yenyewe.”

Mungu pia anachukia michezo ya mapenzi soma Isaya 57:4-5 “Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani, juu ya nani mmepanua vinywa vyenu, Na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo; ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi….. Wachumba wengi hawajui haya kwa sababu si makanisa yote yanayofundisha maswala ya mahusiano ya wachumba kimpana.

Mpaka hapa tunaamini umeshajua hasara za jambo hili  na utazijizuia kabisa kulifanya. Michezo ya mapenzi ni pamoja na kunyonyana ndimi, kushikana sehemu ambazo zinaamsha ashiki ya mapenzi kama sehemu za siri, matiti, kiuno nk, pamoja na kuangalia picha za ngono. Katika kipindi ambacho tumemtumikia Mungu kupitia vijana tumejifunza na kukutana na kesi mbalimbali za aina hii na kuona namna Shetani anavyovuruga mpango wa Mungu kwa vijana. Mwenye sikio na asikie neno ambalo Roho wa Bwana awaambia vijana ili kulida kusudi la ndoa.

Ni imani yetu kwamba mambo haya nane yameongeza ufahamu na hivyo kuwa maarifa ya kutosha kukusaidia kuenenda kwa mapenzi ya Mungu katika kipindi cha uchumba.
Bwana awabariki
imeandikwa na 



Patrick & Flora Sanga

Patrick Sanga ministries.

....****MWISHO****....



NGUVU ILIYOSITIRIKA NDANI YA KUSOMA VITABU
Utangulizi
Kitu kinachoamua kiwango cha uhuru kwenye maisha yako ni kiwango cha ufahamu ulichonacho
Kiwango cha kutokuwepo kwa giza kinaamuliwa na kiwango cha uwepo wa mwanga (Mwanga unapokuwepo kwa wingi zaidi basi giza huwepo kidogo zaidi)

Uko jinsi ulivyo kwasababu ya kiwango cha ufahamu – Ukiongeza ufahamu, utajiongezea uhuru!

Maandiko:
Yohana 8:32

Mifano:
Allegory of the Cave by Plato
Kufikiri jambo usilolijua
Kusoma vitabu ni moja ya njia (njia kubwa sana) ya kuongeza uhuru kwenye maisha yako

Mwanaharakati # 1. Danieli
Rejea Danieli 9:1-3 Kwa kuvisoma vitabu” (Greek: Biblia= books)
(Yer 25:11-1229:10; 30:18; 2Nyakati 36:21)
ü Alikuwa na miaka 15  wakati wa utumwa
üAlikuwa mshauri wa wafalme wanne/awamu nne
          605 K.K Taifa lilichukuliwa utumwani 
          538 KK Ufunuo/Uamsho ndani ya moyo wa Danieli (mwaka wa 67) na mwaka wa 68 taifa lilipokea uhuru.
Kimsingi, taifa lilipaswa kukaa utumwani miaka 70 = kusoma vitabu kuliharakisha uhuru.
Utimilifu wa harakati: Ezra 1:1-6

Mwanaharakati # 2. Musa
Rejea Kutoka 2:11-15
(Mwanzo 15:12-14)
Misimu:
Utumwa & Mateso: miaka 400 ya hali ya ukiwa katika nchi ya ugeni
Uhuru & Mafanikio – kipindi cha utoshelevu:
Rejea
MDO 7:22-30; Kut 12:40-41
Utumwa wa Israeli (Misri) ulidumu kwa muda mrefu kwasababu haukuwa na hamasa ya vitabu (was not book inspired)

Mwalimu Nyerere na Uhuru wa Tanganyika
Baada ya vita kuu za dunia (WW I&II), nchi ya Ujerumani ilipoteza sehemu kubwa ya makoloni.
Umoja wa mataifa uliiweka Tanganyika mikononi mwa Uingereza kwa uangalizi
Tanganyika ilipaswa kujiandaa kujitawala na wakati ilipokuwa tayari ilipaswa kuomba uhuru wake
Masharti hayo ya Umoja wa Mataifa kwa  Uingereza yalikuwa kwenye mfumo wa maandishi
Ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndiye alipata fursa ya kusoma na kuongoza harakati za uhuru

Hitimisho:
Msingi wa Tanganyika umo kwenye usomaji wa vitabu = Tanganyika ilijengwa kwa kusoma vitabu, itatunzwa kwa kusoma vitabu!


                                                 PASTOR; JAMES KALEKWA

....****MWISHO****....


ONGEZA TIJA KWA KUISHI MAISHA YANAYOONGOZWA NA KUSUDI LA MUNGU - (ISAYA 46:9-10, MITHALI 19:21)
Seminar Outline:
¢Day 1: Dhana ya kusudi la Mungu (The concept of God’s Purpose)
¢
¢Day 2: Kutambua kusudi la Mungu kwaajili ya maisha yangu binafsi (Discerning God’s purpose over my personal life )
¢
¢Day 3: Kutoka kwenye ufahamu kuelekea kwenye matendoUtekelezaji wa kusudi la Mungu (From knowledge to Practice: Actualization of God’s purpose )

Day 2: 
Kutambua kusudi la Mungu kwaajili ya maisha yangu binafsi
¢Kila mtu yupo duniani kwa kusudihakuna aliyeko kwa bahati mbaya. (Haijalishi anajua ama hajui ) “Ignorance of the purpose does not cancel it.” Myles Munroe
¢Kuna ombwe (vacuum) duniani ambalo umekuja kulijaza. Kuna uhitaji ambao ni wewe ndiye umekuja kuutimiliza.
¢Wewe si bahati mbayasi majaribio wala si tukio lisilo kusudiwa (ajali )… Upo kwa kusudi.
Sura mbili za kusudi la Mungu
¢Kusudi la Mungu la ujumla kwa wanadamu wote (Corporate purpose )
ü Ref: Mwanzo 1:26-29; Mwanzo 2:7-8
¢Kusudi la Mungu kwa  mtu binafsi (Individual purpose )
Namna ya kujua kusudi la Mungu kwa mtu binafsi
¢Kupitia ndoto Ref: Mwanzo 37:5-7, 9-11
¢Maono
üWakati akili inafanya kazi Ref: Luka 1:30-38; Yer  1:4-9
üAkili haifanyi kazi (Trance ) Ref:
üHalf way Ref: MDO 26: 19, 15-18
¢Kupokea ufahamu – Rhema (neno la Mungu lililovuviwa kwa mtu binafsi) Ref: Dan 9:2
¢ Msukumo kutoka kwenye mazingira Ref: Kut 2:11-12; MDO 7:23-25
Maswali muhimu
¢Je, kuna jambo amabalo linaibukaibuka maishani mwako hata kama unajaribu kulipotezea? (It keeps on surfacing )
¢Je, kuna jamabo ambalo upo radhi kulifanya hata pasipo malipo yoyote (poshomshahara n.k)
¢Je, kuna jamabo ambalo ukilifanya huwa unasikia ridhiko la haki ya juu sana? (Unasikia hali ya ukamilifu - satisifaction )
¢Je, kuna jambo ambalo kila ukilitazama unaona ni kama vile ni wewe peke yako unapaswa kulifanya? As if watu wengine wanaofanya wanatega
?¢Jambo gani ambalo huwa ukilifanya huwa kuna matokeo makubwa wakati umetumia uwekezaji kidogo sana (Watu wengine watadhani umetumia mudanguvu na uwekezaji mwingi )
¢Je, kuna jambo ambalo moyo wako unawaka kulielekea? (You are passionate about it )
Tafakari Muhimu
¢Allegory ya Dr. Stephen R. Covey
¢Allegory ya msafiri
¢Legacy – alama ya miguu kwenye mchanga wa historia.
¢Historia ya marehemu
¢Yeremia20:9

Day 3: 
Kutoka kwenye ufahamu kuelekea kwenye matendoutekelezaji wa kusudi la mungu  
¢Utafiti mdogo wa maisha ya watu hamsini wenye alama kwenye maisha
¢Kuna pattern – (mtiririko fulani unaofanana ) inafanana kwenye maisha ya watu hawa
¢The James Purpose Model
Kusudi
Maono/Dira
Utume/Dhamira
Mipango
Malengo
Mikakati
Orodha ya mambo ya siku kwa siku
1. Maono/DIRA
¢Mithali 29:18, “ Pasipo maono watu huacha kujizuia (huvuka mipaka/hukosa kuwa na adabuhuangamia)…”
Maono ni nini?
¢ Mashindano ya kilimo kwa trekta
¢Habari ya msafiri
¢Mashindano ya mpira wa miguu pasipo miimo miwili kila upande wa uwanja (magoli)
Maono vs Matamanio
¢Manufaa- kwa mtu binafsi au kwa jamii? Mf: kununua gari, kujenga nyumba, n.k
¢Mahitaji- Je, baada ya kujitaabisha kote huko utakuwa umekidhi mahitaji ya nani?
¢Legacy – Unataka kuacha kitu gani baada ya kuwa umeondoka duniani?
¢“There are miracles in life I must achieve, but first I know it starts inside of me” Robert Kelly
Maono: Ushauri kutoka kwenye moyo wa Mungu
Habakuki 2:3, “… Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao…”
¢Maono HUANDIKWA
¢Maono huwekwa WAZI (yenye kueleweka)
¢Maono huwekwa WAZI (husomea- legible)
¢Maono ni LAZIMA yatimilike
2. UTUME/DHAMIRA

3. MIPANGO
¢Kwa muda miaka 2,3,4 hadi 5
¢MAONO ni jambo kubwa & pana – linahitaji kukamilishwa hatua kwa hatua.
¢Kutoka kwenye picha kubwa (MAONO)
üKuongeza kipato kwa 35%
üKukuza uwezo wa kibiashara ya mazao yatokanayo na mifugo (ngozimaziwakwatomanyoya n.k)
üKutengeneza soko-mtandao na usambazaji nchi za Afrika Mashariki
üKuongeza idadi ya watu wanaofikiwa na huduma zetu kwa 40% Kanda ya ziwa
4. malengo
¢Kila mwaka/msimu (mwaka wa fedha, mwaka wa kawaida, mwaka wa masomo)
¢Kutoka kwenye malengo makubwa
¢Gawanya mipango (split) katika shughuli za mwaka mmoja TU!

SMART
Specific – Mahususi
*Lazima ukubali hutofanya KILA KITU!
*Eneo – kijiografiakimtandaokisoko
*Watu waliokusudiwa/wateja/walengwa
Mfano:
 Kuchapisha na kusambaza vitabu vya hadithi za Biblia kwaajili ya watoto kwa makanisa ya kiinjili na kipentekoste mkoa wa Mwanza.

SMart
Measurable – Hali ya kupimika
*Idadi
*Hali (mabadiliko kwenye maisha)
Mfano:
 Kuchapisha na kusambaza vitabu 60,000 vya hadithi za Biblia kwaajili ya watoto kwa makanisa 175 ya kiinjili na kipentekoste mkoa wa Mwanza.
SMArt
Attainable – Je, lengo linafikika?
*Je, inawezekana kuchapisha vitabu 60,000?
*Je, inawezekana kusambaza vitabu?
*Je, kuna makanisa 175 ya kiinjili na kipentekoste mkoa wa Mwanza?
*Kuna rasilimali kuwezesha hilo (watu, nyenzo/vifaafedha) AU inawezekana kuzitafuta
SMARt
Realistic – Yenye kuakisi uhalisia na ukweli
*Mazingira – miundombinu, logistics, kijiografia
*Muda na majukumu
*Umahalishaji (contextualization) – lazima kuakisi mahali
*
SMART
Time bound – Ukomo wa muda
*Jambo lisilo na ukomo wa muda huwa haliishi kwasababu HALINA mwisho!
MFANO:

 Kuchapisha na kusambaza vitabu vya hadithi za Biblia kwaajili ya watoto kwa makanisa ya kiinjili na kipentekoste mkoa wa Mwanza ifikapo Desemba 2017.
5. Mikakati
¢Ni lugha yenye asili yake kwenye jeshi na uwanja wa mapigano
¢Ni mbinu, njia, namna ambazo hufanyika ili kufikia malengo (SMART)
¢Kumbuka: Mikakati ni njia tu, si mwisho (they are just means, not end in themselves)
¢Mikakati inaweza kubadilikakuunganishwakuahirishwakuboreshwa ili kufikia lengo
6. Mambo ya siku kwa siku (To do list)
*Shughuli za utekelezaji za siku kwa siku ili kufikia mipangomalengo kisha maono!
Mfano:
*Kuandika wazo la mradi (concept note) – July 2014
Kubainisha wadau wa mradi na kuwashirikisha wazo la mradi – August – October 2014
*Kuandika andiko la mradi (project proposal/plan)- October 2014- Jan 2015
*Kuandaa mafundisho katika mfumo wa hadithi na picha Jan- October2015


BY JAMES KALEKWA

....*****MWISHO*****....



SEHEMU TATU ZA SADAKA IGUSAYO MOYO WA MUNGU

Kutoa miili yetu kama sadaka na dhabihu takatifu iliyo hai.

Kutoa muda wako kama dhabihu takatifu iliyo hai ili ikamfanyie yeye manukato.

Kutoa mali na fedha zako kwa ajili ya kumtumikia BWANA.

Katika maeneo yote haya Mungu alifanya ili mwanadamu afurahie uzuri na uaminifu wa Muumba wake, na anafurahi sana kuona mwanadamu anashiriki pamoja naye na kumshirikisha katika kila jambo ampalo.

Kutoa miili kama dhabihu iliyo hai ya kumpendeza Mungu 

Maandiko matakatifu katika kitabu cha Warumi 12:1 yanasema “Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Sehemu ya maandiko haya ni sehemu inayoonyesha msisitizo juu ya nini ambacho Mungu anafurahishwa kuona tunakifanya katika kuishi kwetu.

Anasema itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, hii umaanisha kuna sadaka zilizo hai na sadaka nyingine ni sadaka zisizo hai mbele za Mungu. Mtume Paulo anazungumza kuwa ili Mungu akukubali ni lazima kutoa mwili wako kuwa dhabihu iliyo hai. Dhabihu iliyo hai katika miili yetu ni kujitoa kwa kila namna na kuruhusu miili yetu itumike mbele za Mungu kwa ajili ya utukufu wake.

Kuitoa miili kuwa dhabihu ni kuruhusu miili yetu kutii na kufuata makusudi ya Mungu, na pia ni kukubali kuishi kwa ajili ya injili. Kama umedhabihu mwili wako mbele za BWANA ni lazima utakuwa radhi kupatwa na jambo lolote kwa ajili ya BWANA na kwenda popote atakapokupeleka na kuacha lolote analokataza na kusema chochote anachokuamuru useme na kutenda lolote atakalo kuambia utende. Wakati mwingine ni kukubali mateso na aibu kwa ajili ya BWANA.

Unapojitoa katika kuifanya kazi ya Mungu kwa moyo na kupenda pasipo kuhimizwa na mtu awaye yeyote hiyo kwa Mungu ni dhabihu iliyo hai, unapofanya kazi ya Mungu kama kuomba, kuhudhuria ibada, kuhubiri/kufundisha, kufanya usafi katika nyumba ya Mungu, kutembelea wagonjwa na wenye shida mbalimbali, kuimba, na kufanya vitu vingi ila kama hautaki kupata sifa za wanadamu bali unafanya kwa ajili ya BWANA hiyo kwa Mungu ni dhabihu iliyo hai.

 Lakini pia anaongezea kusema takatifu ya kumpendeza Mungu. Huku ni kujitoa huku ukiwa na moyo safi mbele za Mungu. Ukitoa dhabihu iliyo hai na katika hali ya usafi wa moyo ni lazima utampendeza Mungu na kujitoa kwako kutakuwa ni ibada yenye maana; watu wengi wamekuwa wakidharau huduma kama kufanya usafi kanisani, kutembelea wenye shida mbalimbali na huduma nyingine ambazo uonekana ndogo ila huku ni kukosa maarifa katika mambo ya Mungu, kwa sababu Mungu anaangalia kama umejitoa kwa kumaanisha huku ukifurahia toka ndani ya moyo wako au unafanya kwa sababu umepangiwa zamu au umelazimishwa na viongozi wako, kama unafanya kwa moyo ni lazima Mungu aihesabu kazi yako kuwa ni kazi iliyo njema na itakuwa ni ibada iliyo njema kwake.

Fanya kila kitu kwa kujitoa kwa moyo na kupenda huku ukifanya ukiwa katika hali ya usafi wa moyo na ukitambua kuwa kila ukifanyacho kwa moyo na kupenda kwa ajili ya BWANA hiyo ni ibada, hata kwa viongozi wa kiserikali wanapofanya mambo katika hali ya usafi wa moyo na kupenda na kufanya kwa ajili ya BWANA, huwa ni ibada yenye maana mbele za Mungu.

Nikukumbushe kuwa kama ni mtakatifu lakini hujatoa mwili wako kuwa dhabihu mbele za BWANA, kwa Mungu hakuna thawabu uipatayo na pia kama unajitoa sana na kufanya mengi sana lakini kama si msafi wa moyo bado unapoteza muda wako na si ibada mbele za Mungu.

Pia ni vyema kufahamu kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na ni vyema kulitunza kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kutoruhusu jambo lolote lile litakalo fanya kujinajisi na kuwa mchafu, kwa kuwa Mungu uketi pamoja na walio safi wa mioyo. Ni lazima mwili usiambatanishwe na kitu chochote ambacho ni najisi. Kuwa dhabihu hai mbele za Mungu ni kuuhua mwili katika mambo ya ulimwengu huu na kuuweka wakfu kwa ajili ya BWANA.

Yesu aliwaeleza wanafunzi wake kuwa wakati wa hukumu wapo wengi watakao simama mbele za Mungu na kusema kuwa Bwana sisi tulijitoa sana kwa ajili ya kazi yako lakini Yesu atawajibu na kuwaambia siwajui, ila wapo watakatifu ambao hawakujitoa ambao uzungumzwa kuwa hawataipokea taji ya kazi yao. 

Kutoa muda kwa ajili ya BWANA

Ni ukweli kuwa muda wako ndiyo mafanikio yako, unavyoutumia ndivyo unaonyesha kama utafanikiwa au utashindwa kufanikiwa. Kwenye sura zilizo tangulia tulitazama kuwa matumizi ya muda vibaya ni kikwazo kikubwa cha mafanikio yako. Ila katika sura hii tutatazama kuwa uchoyo wa kumnyima Mungu muda ni kikwazo cha mafanikio ya mtu pia.

ukitazama umuhimu wa mawasiliano kwa wapenzi walio ndani ya ndoa na hata wanaokaribia kuoana, utagundua kuwa mazungumzo imara ya mara kwa mara ndio ubora wa mahusiano na hata ndoa kwao. Na ukimpatia mpenzi wako muda mdogo au ukimnyima kabisa muda wa kuzungumza nawe ni lazima utakuwa unaelekea kwenye hatari ya kuvuruga mahusiano yako au ndoa.

Jambo hili linauhusiano sana na Mungu wetu kuwa anapenda tuwe na muda naye na kuzungumza naye na hata kufurahi naye, ila tunapomnyima muda wa kukaa nasi ni kujitengenezea maangamizo yetu wenyewe na wakati mwingine ni kuvunja ukaribu kabisa naye. Kama uwezavyo kumtengea mpenzi wako au rafiki zako muda wa kuzungumza nao ndivyo unapaswa kumtolea Mungu sadaka ya muda wako. Fahamu ya kuwa muda unaoutoa mbele za Mungu ni sawa na sadaka na kama ukitoa vyema na kwa moyo wa kupenda ni lazima Mungu akubariki.

Waefeso 5:15-16 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.” Tuna wakati mdogo sana ila ni lazima tuwe makini tunavyoutumia, epuka kutumia muda wako kama wasiomjua Mungu wanavyoutumia, kwa kuwa wao hawana hata muda wa kukaa na Mungu hata kidogo, ila kama watu wenye hekima za Mungu ni vyema kuukomboa wakati(kufanya mambo ya maana tu ambayo ni mema hata mbele za Mungu)

Visingizio ni ishara ya kupotea, epuka kila wakati kutoa visingizio kwa kuwa hivyo vilikuwepo, vipo na vitaendelea kuwepo ila waweza kuvishinda kwa kujikana wewe mwenyewe. Kuna watu ushindwa kumfanyia Mungu ibada kwa kuwa na visingizio kuwa hawana muda, muda huwa haukamatiki mkononi, na kama ukisubiri kuupata muda kamwe hautoweza kuupata, ila ukiamua kuutumia uliopo ni lazima utafaulu kufanya hata yasiyowezekana.

Acha visingizio kuwa una mambo mengi kwa kuwa hayatakuja kutokea yakawa machache ili upate muda wa kukaa na Mungu wako, pia ukisema una ratiba ngumu inayokunyima muda na Mungu ujue kuwa haitakuja tokea hiyo ratiba ikawa rahisi mpaka umeirahisisha kwa kuchukua maamuzi magumu ya kuwa na muda na Mungu.

Jiulize kuwa mbona mambo mengine unafanya lakini kwenye suala la Mungu tu ndipo unakosa muda, hii ni ishara ya kuwa Mungu kwako si muhimu kama vilivyo vitu vingine. Ni vyema kuweka msimamo wako wa kuwa na muda wako na Mungu na epuka kutokea kitu kingine kukuvurugia. Kama ilivyo kwa mtu wa karibu yako hauoni raha akiwa mbali au usipo wasiliana naye, ndivyo wapaswa kujisikia kwa Mungu kama haujawasiliana naye au kumtafuta na uhuzunike na kuugua sana.

Kama mtu mwenye shauku ya kumjua Mungu na kufanikiwa katika mambo yote ni lazima utumie vyema muda wako, kwa kuwa na ratiba ya kuhudhuria ibada zilizopo, na kuwa na ibada yako binafsi ambapo utamsifu, kumuabudu, kujifunza neno na kuomba Mungu.

Mathayo 26:40-41 “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja. 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho I radhi lakini mwili ni dhaifu”

Yesu anawaambia wanafunzi wake wangekesha hata saa moja, ni vyema kufanya jambo hili kudumu na BWANA hata saa moja kama mambo ni mengi kwa kuhudhuria ibada na wakati mwingine saa laweza likawa jingi ila Mungu anajali sana muda ulioweka kuwasiliana naye.

Muda ni sadaka ambayo unapaswa umtolee Mungu na epuka kutumia muda wote ndani ya siku pasipo kumpa BWANA muda wake.

Kumtolea Mungu fedha na mali. 

Eneo jingine lililo la muhimu sana katika maisha ya mwamini ni eneo la utoaji wa fedha na mali kwa ajili ya Bwana. Eneo hili ni muhimu sana kwa kuwa ni sababu kubwa sana ya Mungu kubariki watu wake na kwa mtu ambaye amekosa uaminifu katika hili eneo ukaaa chini ya laana ila kwa aliye mwaminifu uwa ndani ya Baraka.

Kuna aina mbali mbali za utoaji wa fedha na mali, aina hizo ni kama:

Sadaka ya kuwasaidia watu walio katika uhitaji.

Hii ni sadaka ya mtu kumsaidia mtu haswa Yule ambaye hana matumaini na hana msaada kwa kutoa vile alivyonavyo na kumpatia. Hii ni sadaka ya upendo kwa kuonyesha kumpenda Mungu na kumpenda Yule unayemsaidia.

Hii ni sadaka ambayo mtu anaifanya mbele za mtu kwa ajili ya Mungu, na ikifanyika kwa mtu kujitakia utukufu wake huwa haina thawabu mbele za Mungu ila ikifanyika kwa moyo wa kupenda na kumtukuza Mungu ni njema na ubeba thawabu kubwa mbele za Mungu.

Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakacho pimiwa.”  Yesu anapotoa neno hili anazungumza na watu walioamini kuwa imewapasa kutoa vitu vyao kwa watu(wenye uhitaji) ila kutoa kwao si bure kwa kuwa ni lazima Mungu atawarudishia tena  kupitia watu,  si kama walivyotoa bali ni zaidi kwa kipimo cha kujaa  na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata kumwagika.

Mfano wa sadaka hii katika biblia ni:

Sadaka ya Rahabu kujitoa na kujihatarisha ili wapelelezi kutoka Israeli wapone.

Kitabu cha Yoshua 2:1-6

Sadaka ya BWANA Yesu kwetu wanadamu.

Kitabu cha Isaya 53

Sadaka ya mjane wa Sarepta kwa Eliya.

Kitabu cha 1 Wafalme 17:13-16 “

Sadaka ya Kornelio kwa watu wenye shida mbali.

Kornelio alikuwa mtoaji sana na aliwapa watu sadaka nyingi sana, kama inenavyo katika Matendo ya mitume 10:2 “mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.

Sadaka ya mtu kujitoa na kutoa vitu vyake vya thamani ni sadaka yenye thamani sana mbele za Mungu na ni ishara ya kuwa mtu anampenda Mungu na yule anayemsaidia.

Sadaka kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Mungu.

Sadaka hii huitwa kwa majina mengi, na wengine huiita sadaka ya lazima. Wengine matoleo, wengine upenda kuiita sadaka ya ibada. Hii sadaka utolewa kila watu wa Mungu wakutanikapo pamoja kufanya ibada, na mlengo mkuu wa sadaka hii ni kuiendeleza kazi ya injili ipate kusonga mbele.

Ni sadaka ambayo utumika kuimalisha miundombinu ya kanisa, na pia kuwa saidia watumishi wa Mungu, na shughuli nyingine nyingi kama ilivyopangwa na kanisa husika la mahali pamoja. Hii ni sadaka muhimu sana na ni ya lazima kwa kila muumini kuangalia kuitoa kila anapokuwepo ibadani.

Hii ndiyo sadaka inenewayo kuwa usiingie nyumbani kwa BWANA mikono mitupu.

Sadaka ya malimbuko.

Hii ni sadaka ambayo ni ya mwanzo wa kila pato ulipatalo katika yale uyafanyayo. Kama ni biashara basi yale mapato ya kwanza ni malimbuko yako kwa BWANA, kama ni kazi huwa mshahara wa kwanza, kama ni mazao uwa yale ya kwanza na vivyo hivyo kwa wanyama. Sadaka hii pia kwa nyakati za leo uwasilishwa kanisani.

Sadaka ya shukrani

Kitabu cha Zaburi 50:14

Hii ufanywa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa lile lililotokea katika maisha liwe zuri au baya.

Mwalimu Mwakasege anaielezea kuwa ni sadaka ya muhimu kuifanya kila wakati unapofanyiwa jambo au unapokumbwa na jambo, na uelezea kuwa hii ni sadaka ya msingi sana kumshawishi Mungu azidishe utendaji wake katika maisha ya mwamini.

 Zaburi 50:5

Matendo ya Mitume 5:1-11

Fungu la kumi.

Malaki 3:8-12

Hii ni sehemu ya kumi ya mapato yako yote uyapatayo, ni  sadaka muhimu sana ambayo pia ipo kwa ajili ya kuiendeleza kazi yake.

–Na Mwl Kelvin Kitaso

....****MWISHO****....





 JE UKIOKOKA UNAJITENGA NA ULIMWENGU??

SHALOM!

NATUMAI UKO SALAMA,LEO TENA KUNA MAADA RAHISI TU HAPA,KAMA UNAWIWA NAOMBA UJADILI KWA MISINGI YA BIBILIA NA NENO LA MUNGU TU

KUNA MAMBO AMBAYO HUWACHANGANYA WENGI WA WAPENDWA,NI MAGUMU KUYASEMEA KWA HARAKA HARAKA BILA KUWA NA MISINGU THABITI!

JE DHAMBI NI NINI?
MACHUKIZO JE?
JE UKIWA NA TAALUMA YAKO KWA MFANO MHASIBU UKIFANYA KAZI KAMPUNI YA BIA NI DHAMBI?

AU WEWE NI MJENZI,UKIPATA TENDA YA KUJENGA ITAKUWA DHAMBI?

AU LABDA WEWE NI MTALAAMU WA KOMPYUTA NA IT,JE UKIITWA KUWATENGENEZEA SITE NA BAADHI YA VITENDEA KAZI UTAKWENDA?

JE UKIINGIA KULA BAA INAKUWAJE?

JE UKIWA MTANGAZAJI WA MEDIA YA KIDUNIA NA WADHAMINI WA KIPINDI CHAKO NI POMBE AU SIGARA,JE UTAACHA KAZI?

NA KWA MFANO UKIPATA SHIDA KAMA MAFURIKO VILE,TETEMEKO AU KUUNGULIWA NYUMBA MOTO, NA MARA WAKAJA TBL KUTOA MISAADA KWA WAHANGA NA WEWE UKIWEPO,JE UTAKATAA AU ITAKUWA DHAMBI UKIPOKEA?

WEWE UNAONAJE?


SABABU ZA KUFELI NA KUSHINDWA

(FACTORS OF FAILURE)

Kwanini watu wa Mungu wanafeli au wanashindwa au wanakwama?
Hili ni swali la muhimu sana ambalo linaweza kuwa kama funguo ya dhahadu katika mlango wa mafanikio a maisha yetu. Kama tukilifungua swali hili vizuri, tutaweza kupata majibu ya matatizo mengi katika maisha yetu sisi watoto wa Mungu. Kulingana na ukweli (Neno la Mungu – Biblia) sisi wana wa Mungu ni “washindina zaidi ya washindi, katika mambo yote (Warumi 8:37;   1Wakorintho 15:57).

Kulingana na Ukweli wa Neno la Mungu, watu wa Mungu tumeshabarikiwa na kukabidhiwa vitu vyote tunavyohitaji kwa ajili ya maisha yetu yote ya mwilini na rohoni (Efe 1:3; 2Pet 13-4). Kama ni ushindi juu ya dhambi na dunia, uwezo huo tumeshapewa na Bwana. Mtu wa Mungu akikumbwa na tamaa za dunia hii, ina maana kwamba, yeye mwenyewe ameruhusu au amekubali kumtii shetani kuliko Mungu (Wagalatia 1:3-4; 1Yohana 2:15-17). Kama ni ushindi dhidi ya nguvu za giza, mapepo na wachawi; Mungu amekwishatupa uwezo huo wa kuwashinda watenda kazi wote wa ibilisi shetani (Wakolosai 1:13; Luka 10:19)

Kama ni ushindi katika afya, tumepewa na tumeponywa tangu damu ya Yesu ilipomwagika msalabani kwa ajili yetu, na kwa kupigwa kwake sisi tulikwishaponywa tayari (1Petro 2:24; Mathayo 8:17). Kama ni jambo la uchimu na utajiri, watu wa Mungu tulkwishafanywa matajiri na Kristo, kwa kifo chake. Yeye alichukua umaskini wetu akatupa utajiri wake (2Wakorintho 8:9; 2Wakorintho 9:11). Kama ni suala la akili an hekima, watu wa Mungu tumekwishapewa uwezo mkubwa wa kiakili na fikra, kwa Roho Mtakatifu wa Mungu anayeishi ndani yetu. Sisi wana wa Mungu tuna akili na ufahamu wa kiungu. (Isaya 11:2; Zaburi 111:10; Matendo 6:8-10; 2Timotheo 2:7)

Kama ni baraka katika mikono yetu, tumekwishapewa na Mungu kwa ajili ya shughuli zetu (Kumbukumbu 28:1-8; Zaburi 1:1-3) Kama ni ulinzi juu yetu na nyumba zetu na mali zetu, Bwana amekwisha waagiza malaika zake watuzunguke kwa panga za moto, farasi, magari ya moto (kufanya ukuta mzito wa moto) kutuzunguka (Zaburi 34:7; 2Wafalme 6:15-17; Zaburi 121:1-8; Zaburi 91;1-11-12).

SABABU ZA KUFELI NA KUSHINDWA

Kila kitu ambacho watu wa Mungu tunachohitaji katika maisha yetu yote ya mwilini an rohoni, tumekwisha kupewa na Baba yetu aliye mbinguni, ili tuweze kuishi maisha ya ushindi katika kila eneo linalotuhusu au linalotuzunguka. Kama ukweli ndio huu basi, kwanini watu wa Mungu wengine wana maisha ya kushindwa na kufeli? Kwanini watu wa Mungu wengine wanaishi maisha ya kuhangaika na kukosa? Ni lazima kuna sababu.

1            KUTOKUJUA
Mungu anasema watu wangu wanaangamia (wanateseka na kuhangaika) kwasababu ya kukosa maarifa (ufahamu na ujuzi wa mambo niliyokwisha watendea) … japo wana bidii nyingi lakini wana bidii bila maarifa (wanapoteza nguvu nyingi katika maisha) (Hosea 4:6;  Warumi 10:2) Ndio maana Paulo alikuwa anawakazania sana wanafunzi wake ili wapate Roho ya hekima na ufunuoili wapate “Kujua“ mambo tuliyokwisha kupewa na Mungu kupitia Yesu Kristo. Alimwambia Timotheo hivi, yafahamu sana mambo haya… (2Tim 2:7).

Ndugu yangu, mambo usiyoyajua, hutaweza kuyapata; hayatatendeka maishani mwako. Kujua ndio mwanzo, ndio ufunguo wa kuyafungulia ili yaweze kuja kwako. ndio maana tunaambiwa Neno la Kristo likae kwa wingi katika mioyo yetu, kwa hekima yote … kuyajua maandiko matakatifu kunatuhekimisha ili tupate ufahamu wa haki zet na baraka zetu (Wakolosai 3:16; 2Timotheo 3:15-17)Ukitaka ufahamu na ujuzi, soma kwa bidii Neno la Mungu. Pata maarifa.

2            KUONA VIBAYA
Kutokujua kunasababisha kuona vibaya. mtu asiyejijua kuwa yeye ni shujaa, atajiona dhaifu. asiyejijua kuwa yeye ni mzima, ayajiona mgonjwa. asiyejijua kuwa yeye ni mbarikiwa, atajiona ni maskini. Soma vizuri habari ya wana wa Israeli kitabu cha Hesabu sura ya 13 na 14 yote, utaona jinsi wana wa Isreali walijiona wao ni kama panzi mbele ya wenyeji wa Kaanani. Hii ni kwasababu hawakujua vizuri na kwa uhalisi, uwezo wa Mungu aliye pamoja nao, japo waliyaona matendo yake ya ajabu. kutokujua kunasababisha kuona vibaya.

Hii ndio sababu iliyomfanya Mtume Paulo atuombea Wakristo tupate kufunguliwa katika macho yetu ya ndani, ili tuweze kuona vizuri, mambo ya rohoni. tukiona vizuri, tutapata ufahamu sahihi wa jinsi tulivo rohoni na jinsi tunavyotakiwa kuwa katika mwili (Waefeso 1:15-19).

Gideon alikuwa anajiona yeye ni dhaifu na muoga lakini Mungu akimuangalia anamuona yeye ni shujaa, na ndio maana Mungu alimwita “ewe shujaa” japo kuwa yeye Gideoni alikuwa katika maficho kwa hofu ya maadui. Soma vizuri habari hii katika (Waamuzi 6:11-14) Bwana akamwambia “enenda kwa nguvu zako”. Maana yake ni kwamba, kumbe Gideoni alikuwa na nguvu za kutosha ndani yake, lakini hakujua! Kutokujua kunaweza kukunyima kusonga mbele. kutokujua kulimfanya ajione mnyonge mbele ya maadui wao. Mungu akusaidie kujiona sawa sawa na yeye anavyokuona na sio kama unavyojiona wewe

Kama utatumia mwanga wa manjano ndani ya nyumba yako, vitu vyote vitaonekana ni vya manjano. Kama ukitumia mwanga mwekundu, vitu vitaonekana ni vyekundu. Vivyo hivyo katika dunia, Yesu anasema kwamba yeye ndiye nuru (mwanga) wa ulimwengu (Yohana 1:7-9) Tukimtumia yeye kuangalia mambo yetu, yataonekana vizuri kuliko tunavyoyaona sasa. Yesu ni Neno (Yohana 1:1-4; Ufunuo 19:11-13). Tumia Neno la Mungu (mwanga bora na halisi) kutazamia maisha yako, utayaona kama Mungu anavyoyaona na si kama wewe unavyoyaona. Kwa Neno la Mungu, Hutajiona mgonjwa bali mzima; hutajiona maskini, bali tajiri; hutajiona dhaifu bali hodari. soma sana Neno la Mungu ubadilishe unavyojiona. Kuona sawa sawa kutakuokoa na jambo lifuatalo.


3            KUWAZA VIBAYA
Kutokujua kunasababisha kutokuona sawa sawa; na kutokuona vizuri kunasababisha kutokuwaza sawa sawa. Kwa lugha rahisi, Kuwaza vibaya ni matokeo ya kuona vibaya. na mtu wa Mungu akitawaliwa na mawazo mabaya juu yake, anasababisha nguvu za Mungu zisifanye kazi juu yake na hiyo inaletakushindwa kimaisha kwa watoto wa Mungu wengi. Sikiliza, mawazo ni daraja lililo katika ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili.
Ndio maana mtu anaweza kusafiri mbali sana kimawazo tu wakati mwili wake upo hapo hapo mlipo. mawazo yakihama, mtu anaweza asiwe anasikia unachosema wala asione unachodhani anaona japo macho yake yako wazi kabisa. Hii ni kwasababu, mawazo yake yamehama; mtu huyo hayupo hapo kimawazo, bali yupo sehemu nyingine kabisa japo mwili wake upo hapo hapo mlipo. Mawazo ni daraja la mambo ya rohoni na mambo ya mwilini.

Mawazo hutawala mambo ya mwili.
Kwa mfano; mtu anayetembea katika barabara ndefu yenye maduka mengi na vitu vingi, bila kuchoka hata kama ni kilometa 5, kwasababu macho yake yanaangalia vitu vingi na mawazo yake yanaona vingi (yako busy). Lakini mtu huyo huyo anapotembea katika barabara nyingine ya urefu ule ule, isiyo na maduka pamoja na vitu vingi vya kutazama, mtu huyo huyo atasikia kuchoka na ataiona safari ile imekuwa ndefu sana kuliko ile ya mwanzo. Tofauti yake ni kwamba, katika safari ya pili, mawazo ya mtu huyo hayakushughulishwa sana kwakuwa macho yake hayakuwa na mambo mengi ya mazuri ya kuvutia kutazamwa; na hali hiyo imesababisha mtu huyo, kujisikia kuchoka katika mwili. Hii inathibitisha kwamba, mawazo hutawala mwili.

Mfano mwingine; mtu aliyebanwa na haja ndogo barabarani, akiangalia kushoto na kulia, akakosa mahali penye choo, mwili wake hutulia. lakini kadri mtu huyu anavyokaribia nyumbani au mahali popote penye choo, mwili wake huanza fujo za kutaka kuachilia ile haja iliyobanwa kwa muda mrefu. kadri mawazo yanavyotambua kwamba hapo karibu kuna choo, ndivyo mwili unavyokosa nguvu ya kuendelea kujibana. mtu huyo akikimbilia chooni na kumbe akakuta kuna mtu chooni, mwili wake, kwa mara nyingine, hukubali kujibana mpaka nafasi ipatikane. Hiyo inaonyesha kuwa, mawazo hutawala mwili.

Mfano mwingine; watu wawili walipigana sokoni. Mmoja akampiga mwenzake kichwa katika upaji wa uso wake. Yule aliyepigwa, alipasuka katika upaji wa uso wake na damu nyingi ikamtoka. Fikiri mwenyewe; upaji wa uso wa mtu wa kwanza umeupasua upaji wa uso wa mtu wa pili, lakini upaji wa uso wa mtu wa kwanza haukupasuka, bali ulivimba tu kidogo. Unadhani tofauti yake ni nini? Jibu: Ni kwasababu, mawazo ya mtu wa kwanza, yalijua tunakwenda kumpiga mtu wa pili kwa kichwa;
kwahiyo, nyama za mwili wa mtu wa kwanza zilikuwa zimeshaandaliwa kwa mawazo ya huyo mtu wa kwanza; lakini mawazo ya mtu wa pili, hayakujua kuwa kuna kichwa kinakuja kutupiga, hivyo nyama za mwili wa mtu wa pili zilikuwa hazijaandaliwa kupokea kipigo; na ndio maana upaji wa mtu wa pili ukapasuliwa na upaji wa mtu wa kwanza. Hii inathibitisha kwamba, mawazo hutawala mwili.

Kwahiyo mtu wa Mungu, Biblia inaposema tugeuzwe fikra zetu, ina maana kubwa sana. Kwasababu, fikra zako zikiwaza vibaya, uasababisha mambo yako ya mwilini kwenda vibaya, hata kama wewe ni mwombaji. Lazima ujifunze kuwaza sawa sawa kama Neno linavyosema kuhusu wewe. Mkumbuke Gideoni, alikuwa anajiona dhaifu na ndio maana alikuwa dhaifu na maisha yake yakawa ya kitumwa. Lakini Mungu alipomwambia kwamba yeye ni hodari na shujaa, Gideoni akageuza fikra zake, akajiona shujaa (kama Mungu alivyokuwa anajiona na sio kama yeye alivyokuwa anajiona mwanzoni).

Mungu hakuwa na haja ya kumpa Gideoni nguvu kutoka mbinguni, balin mawazo mazuri ya ushindi yalitosha kumpa Gideoni nguvu za ajabu. kwa lugha nyingine, mawazo mazuri ya kishujaa, yalifungulia nguvu za Mungu zilizokuwa ndani yakena Gideoni, akaweza kuwaongoza Waisraeli katika ushindi mkuu dhidi ya adui zao. Tena kitu cha kushangaza, askari 300 tu wa Israeli waliwapiga maadui waliokuwa zaidi ya elfu 30.  (Soma vizuri habari hii katika kitabu cha Waamuzi sura ya 6 na 7).

Kwahiyo, ukujiona dhaifu, utasababisha udhaifu katika maisha yako. Ukijiona maskini au huwezi, utasababisha balaa, nuksi, mikosi, kushindwa na ufukara katika maisha yako au katika biashara yako au shamba lako au mifugo yako. Badilisha unavyojiona, utajikuta unabadilisha unavyojiwazia. Tumia Neno la Mungu kugeuza fikra zako na kuzifanya mpya, kuanzia sasa. Kulingana na Biblia, wewe ni shujaa na si dhaifu (Waefeso 6:10); wewe ni mzima na si mgonjwa (2Petro 2:24); wewe ni tajiri na si maskini (2Wakorintho 8:9); wewe ni huru na si mfungwa katika nguvu za giza (Wakolosai 1:13).


Tumia Neno la Mungu kugeuza fikra zako na kuzifanya mpya, kuanzia sasa. Badilisha unavyojiona, utajikuta unabadilisha unavyojiwazia. Ukijiwazia mawazo mazuri ya ushindi na mafanikio, ndivyo utakavyosababisha katika mwili wako, kwasababu mawazo hutawala mwili.

Ndio maana Neno la Mungu linasema; fikra zetu zigeuzwe na kufanywa upya kwa Neno la Mungu (Warumi 12:2; Waefeso 4:17-23-24). Hii inatokana na kanuni ya kwamba, mawazo ya nguvu ya kutawala mambo ya mwili. Ndio maana mtu wa Mungu inakupasa uwe na mawazo safi. Mungu Baba yako mwenyewe anakuwazia mawazo mazuri ya matumaini (Yeremia 29:11) Nakushauri ujifunze kujiwazia mawazo mazuri.

Usijione tena duni au dhaifu au mtu wa kushindwa au mtu wa kuugua au sio mzuri. Hapana, jione tofauti; jione mzuri, jione unaweza, jione una nguvu za kushinda, jione hodari na shujaa, jione kuwa wewe ni mzima hata kama hali ya afya yako ya mwili si nzuri, jione tofauti. Jione wewe uko huru hata kama huwa unajijua unasumbuliwa na nguvu za giza. Badilika! Jione tofauti. Jione wewe ni tajiri, mtu wa mafanikio. Mawazo ni ufunguo! Ukijiona vizuri (kama Mungu anavyokuona na si kama wewe unavyojiona) utapona katika tatizo linalofuata.



4            KUONGEA VIBAYA
Kama tulivyoona, ufahamu husababisha kuona; na kuona husababisha kuwaza; namawazo husababisha maneno. Ukiona vibaya, utawaza vibaya; na ukiwaza vibaya utaongea vibaya. kuna nguvu ya ajabu sana katika maneno yetu. maneno ya nguvu ya kuumba. Biblia inasema ulimwengu uliumbwa kwa Neno la Mungu (Waebrania 11:3) Mungu aliumba vitu kwa kusema tu. Na kwakuwa Mungu ametushirikisha tabia ya uungu (Zaburi 82:6; Yohana 10:34; 2Petro 1:3-4) Kwahivyo basi, maneno yako yana nguvu ya kuumba. Hivyo, uwe mwangalifu unaongea nini au unajitamkia nini.
Chanzo cha nguvu ya maneno.
Nguvu ya maneno inatoka wapi? Maneno ni malighafi ambayo hutumiwa na Roho Mtakatifu au na roho wachafu (mapepo). Biblia inasema kwamba, kila andiko lenye pumzi ya Mungu (Roho) huwa Neno zuri la kufundishia na kuadabisha maisha ya watu. (2Timotheo 3:16-17) … na Neno la Mungu li hai na lina nguvu (Waebr 4:12) Hii ina maana kwamba;

                                     Andiko  +  Roho  =  Neno (Uhai na Nguvu)
                                            (2Kor 3:6)     (Mwa 2:7)    (Ebr 4:12)

Kwahiyo, Neno likivikwa “roho” linakuwa hai na linaweza kwenda kutenda kazi fulani. Ndio maana Mungu alisema kwasababu Neno langu ni Roho (yaani limevikwa au limejazwa Roho Mtakatifu), hivyo basi … Neno langu li hai, tena lina nguvu … na litokalo katika kinywa changu, halitarudi mpaka limeyatimiza mambo niliyolituma kufanya (Yohana 6:63; Waebrania 4:12; Isaya 55:10-11).

Hii ina maana kwamba, Neno la Mungu hupewa uhai na nguvu kutoka katika Roho Mtakatifu aliyelivika hilo Neno. Kwahiyo, unapojibariki kwa maneno mazuri, Roho Mtakatifu huja kulivika uhai na nguvu hilo neno lililotoka katika kinywa chako, ili liwe hai na liweze kukutimizia kile ulichotamka (ulicholituma kufanya). Kwa mfano; siku moja Bwana Yesu aliulaani mti na baada ya masaa kama 8 hivi, ule mti ulikufa!(Marko 11:12-14; 20-23) Tunaona Yesu hakutumia shoka au msumeno kuuua ule mti, bali alitumia maneno yake tu na ule mti ukafa.

Yesu alituma neno tu na Roho Mtakatifu akavamia lile neno na kulipa nguvu na uhai, hata likaweza kutenda kile ambacho Yesu amelituma kufanya; yaani kuua. Kuna nguvu ya ajabu sana katika maneno, kwasababu ya roho zinazoweza kuvamia hayo maneno na kuyafanya hai na yenye nguvu. Ndio maana Biblia inasema mtu hushibishwa maneno ya kinywa chake na mauti na ulimi huwa katika uwezo wa ulimi; na wote waupendao, watakula matunda yake. (Mithali 18:20-21). Hivyo basi, ukitamka maneno mabaya, Roho Mtakatifu hawezi kuja kulipa hilo neno lako uhai na nguvu; kwasababu Mungu habariki udhaifu au laana (negative words). Mungu anabariki maneno ya baraka tu (positive words).

Kwahiyo; ukijitamkia maneno ya mabaya ya udhaifu, laana, balaa na kushindwa, mapepo wachafu huja na kuvamia hayo maneno na kuyapa uhai na nguvu, na yatafanya kazi maishani mwako kukushibisha ulichotamka kwa ulimi wako mwenyewe. Umetegwa kwa maneno ya kinywa chako na umekamatwa kwa maneno ya midomo yako (Mithali 6:2).

Watu wengi hawajui kwanini Yesu alimtaka Petro akiri kwa  kinywa chake, tena mara tatu, kwamba anampenda Yesu (Yohana 20:1-19). Jiulize, jibu la kwanza la Petro, halikumtosha Bwana Yesu? Yesu hakuridhika? Kumbuka kwamba, Petro aliwahi kumkana Bwana Yesu kwa kinywa chake, tena mara tatu, ya kwamba yeye Petro hamjui Yesu. Hayo maneno ya Petro yalianza kuzaa matunda. Tunamuona Petro, baada ya kifo cha Yesu, Petro alianza kupata mawazo ya kuziridia nyavu zake za uvuvi wa samaki, kazi ambayo Yesu alishamwachisha.

Hayo yalikuwa matunda ya maneno yake; kwa lungha ya leo, tungesema Petro alikuwa anaacha wokovu!  Ndio maana ilimbidi Yesu kumfuata Petro na ndugu wanafunzi wengine, kule baharini. Na alipowapata, Yesu akaanza kumtamkisha Petro mara tatu ili kumsaidia Petro aweze kufuta maneno yake mabaya ya laana. Maneno ya kinywa chako yana nguvu ya kusababisha kile unachosema kitokee katika ulimwengu wa mwili, kwasababu kuna roho zinazowinda maneno ili zivae hayo maneno ya kuyaleta mwilini. Hivyo uwe mwangalifu unatamka nini. Ukitamka laana, pepo wachafu watakusaidia na utapokea laana. Lakini ukitamka baraka, Roho Mtakatifu pamoja na malaika (Waebrania 1:14) watakusaidia, na utapokea baraka, ushindi na mafanikio.

Ikikulazimu kutamka maneno ya udhaifu, usiyaache yananing’inia hivyo hivyo, mapepo yatakushibisha; bali hakikisha unayafuta kwa maneno mengine mazuri ya naraka na ushindi. Kwa mfano; Umetoka kwenye mtihani mgumu sana, watu wakikuuliza habari za mtihani, unaweza kuwajibu kwa ushindi tu kwamba ‘mtihani ulikuwa mzuri tu’ ingawamoyoni unajua mambo yalikuwa magumu. Lakini ikikulazimu, wee sema tu kwamba ‘mtihani kwakweli ulikuwa mgumu sana, lakiniMungu atanipigania’. Hapo utakuwa umeshafuta ule udhaifu kama Petro.

Kama unaumwa na hali bado si nzuri, unaweza kusema ‘namshukuru Mungu ninaendelea vizuri’ japo wewe binafsi unajua hali bado ni ngumu. Huo ushindi na uzima unaoukiri, utakuwa malighafi kwa Roho Mtakatifu, kukuletea uzima wako katika mwili. Lakini ikikulazimu, wee sema tu hali ‘hali yangu bado lakini Mungu ataniponya’. Hapo utakuwa umefuta ule udhaifu ulioutamka. Hili tunajifunza kwa Bwana Yesu mwenye; alisema udhaifu lakini hakuacha maneno yake dhaifu yananing’inia, bali aliyafuta kwa kutamka maneno mengi ya baraka na ushindi kwa nyuma yake.

Kwa mfano; Yesu aliwahi kusema “ulimwenguni mnayo dhiki (hili si neno zuri. lakini kahuishia hapo, bali alifuta udhaifu/kushindwa kwa neno la ushindi, akasema) lakinijipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu (yaani; alikuwa anatuambia kwamba, kama yeye ameshinda, na sisi tutashinda tu) Yohana 16:33. Pia aliwahi kusema “mwana wa Adam atauwawa (halafu akafuta kwa kusema) lakini siku ya tatu atafufuka (Marko 16:21).  Ndio Mungu anasema “aliye dhaifu na aseme mimi ni hodari” (Joel 3:10). Kwahiyo; kama unataka kubadilisha hiyo hali uliyonayo, usiseme jinsi hali ilivyo, bali tamka vile unavyotaka hali yako iwe katika mwili.

Tumia nguvu ya maneno yako, hata kama hali si ya kutia moyo sana, lakini usiseme wewe ni dhaifu, bali  sema ‘mimi ni hodari katika jina la Yesu’ (Yoel 3:10); usiseme wewe ni mgonjwa, sema ‘mimi ni mzima katika jina la Yesu’ (1Petro 2:24); usiseme wewe ni maskini, bali sema ‘mimi ni tajiri katika jina la Yesu’ (2Wakorintho 8:9); usiseme kwamba hutaweza, bali kiri kwamba ‘mimi ninayaweza yote katika Kristo anitiaye nguvu’ (Wafilipi 4:19). Hivyo ndivyo watu wa imani tunavyoshinda na zaidi ya kushinda katika dunia hii hii mbovu. Kwwahiyo umegundua kwamba, watu wa Mungu wengi wanafeli na kushindwa kimaisha kwasababu ya maneno yao wenyewe.


5            KUOMBA VIBAYA
Jambo jingine linalosababisha watu wa Mungu ambao ni wabarikiwa lakini wanaishi maisha ya shida na taabu ni suala zima la kutokuomba ipasavyo au kuomba vibaya.Katika sura ya tatu na sura ya nne, nimeongelea sana juu ya watu wa Mungu kutokuwa waombaji. Katika pointi hii, siongelei kutokuomba, bali naongelea kuomba vibaya. Kwahiyo utagundua kwamba, baadhi ya watu w Mungu, wana bidii sana katika kuomba lakini bado hawapokei yale wanayoyaomba, kwasababu wanaomba vibaya. Mungu anailalamikia hii hali kwa kusema kwamba, mnaomba lakini hampati, kwasababu mnaomba vibaya (Yakobo 4:3).

Mtume Paulo pia anasema watu wa Mungu wanabidii sanakatika mabo ya Mungu lakini si katika maarifa (Warumi 10:2; Hosea 4:6). Maana yake ni kwamba; watu wa Mungu wanavuja jasho sana lakini matunda wanayoambulia ni kidogo. Yesu naye anasema ninawashangaa, mbona mnavyohangaikia maisha, kula na kunywa na kuvaa, kama mataifa wasi na Mungu (Mathayo 6:31-32)

Maana yake ni kwamba, wana wa Mungu hatutakiwi kuhangaika na kuhenyeka duniani kwa ajili ya maisha na mahitaji yake kama mataifa, bali tunatakiwa kupata msaada wa Mungu katika kila eneo la maisha yetu, kwasababu sisi ni wa thamani kuliko maua na ndege na yeye Mungu ndiye anayetuhudumia sisi (kama anavyowahudumia ndege na maua). Maneno haya hayamaanishi tusiende kulima na kufuga au kusomana kufanya kazi; haimaanishi tusiende kufanya biashara, NO! Maana yake sio hiyo, bali alikuwa na maana hii; twende tukafanya kazi kwasababu kufanya kazi ni agizo la Mungu;

Lakini, katika kafanya kazi kwetu, tuudhihirishie ulimwengu kuwa, sisi wana wa Mungu, tuna msaada wa Mungu katika kila tunachofanya. Kama Mungu anakusaidia katika kila unachofanya, hautakiwi kuhangaika na kuhenyeka. Msaada wa Mungu unakusaidia kupata mahitaji yako yote katikati ya dunia hii mbovu iliyoharibika. Lakini ukiangalia maisha ya baadhi ya watoto wa Mungu, ni ya kuhangaika na kuhenyeka kama vile hatuna Mungu. Hali hiyo haitutofautishi na mataifa wasiomjua Mungu. Mungu anataka iwepo tofauti kati ye watoto wa Mungu na watoto wa shetani (1Yohana 3:10; Kutoka 11:7; Kutoka 8:23; Kutoka 9:4)

Kwahiyo, Mungu anatamani kuona watoto wake tunarithi baraka zote alizotuwekea katika ulimwengu wa roho. Mungu anatamani sana kuona damu ya Yesu imemwagika kwa thamani yake, kwamba watoto wake tumepata vyote ambavyo damu ya yesu ilitununua navyo. Lakini sivyo ililivyo; na moja ya sababu ni kwamba, watu wa Mungu wanabidii sana katika mambo ya Mungu lakini si katika maarifa (Warumi 10:2; Hosea 4:6). Maana yake ni kwamba; watu wa Mungu wanavuja jasho sana lakini matunda wanayoambulia ni kidogo. Katika pointi hii, siongelei kutokuomba, bali naongelea kuomba vibaya.

Kwahiyo utagundua kwamba, baadhi ya watu wa Mungu, wana bidii sana katika kuomba, kwenye mikesha wapo, kwenye kufunga swaumu, wapo; lakini bado hawapokei yale wanayoyaomba. Hii ni kwasababu wanaomba vibaya. Mungu anailalamikia hii hali kwa watoto wake kwa kusema; mnaomba lakini hampati, kwasababu mnaomba vibaya (Yakobo 4:3).


Tunakosea wapi katika kuomba?

a)   Kuomba Mambo manyonge (Isaya 41:21)
     Isaya 43:26, Zaburi 2:7-8,  2Wakorintho 9:6, Wagalatia 6:7

b)   Kuomba Pasipo uhakika (imani) (Yakobo 1:5-7)
Waebrnia 11:1, 6,   Waebrania 10:38

c)    Kuomba nje ya mapenzi ya Mungu  (1Yohana 5:14-15) < Kitu / Muda / Mahali >
Mathayo 26:36-44, Warumi 8:26-27;  Waefeso 6:18,    Yuda 1:10

d)   Kuomba kwa kukatisha (1Wathes 5:17)
(1) Luka 18:1-7,  (2) Yakobo 5:17-18  (1Waflme 18:41-44), (3) Wagalt 1:6 / 4:19
(Wakolosai 4:2,   Waefes 6:18)

e)   Kuomba kwa msimu  (Walawi 6:12-13)
Luka 10:1, 9, 17;  Mathayo 17:14-16-21; 1Wafalme 20:19-22
Mfano; Mathayo 26:36-46 Linganisha na Matendo 2:43-47, 42 / 3:1- 4:1-13-18-20-31 

f)    Kuomba bila kumpinga shetani  (Yakobo 4:7)
Ufunuo 5:8-10, Ufunuo 1:5-6,  1Pet 2:9
Mwanzo 1:26-28,  Zaburi 8:4-8, 1Yoh 4:13,17,
Mathayo 28:18;  Luka 10:19, Yeremia 1:10/ 51:20
Waefes 6:12-13, 10-11;   Joshua 1:3, 6-9, 5.

g)    Kumpinga shetani wakati una vitu vyake (Yohana 14:33)
Yakobo 4:3-7;  Marko 11:25-26;  Mathyo 6:14-15;  Isaya 59:1-2;  Yohana 9:31.

....****MWISHO****....




KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 1


Naamini uko poa na unaendelea vizuri!!
Naamini bado una akili timamu na unajielewa zaidi una hofu ya Mungu ndani yako (Kama sivyo basi hapa kwako ni pagumu)
"KUSIFU" na "KUABUDU" ni ibaada kamili mbele za Mungu,msingi wa ibaada zote na inayopaswa kufanywa kwa makini,ustadi na furaha tele kwa ajili ya Mungu na Ibaada hiyo inawapasa wanyofu wa mioyo!!
KUSIFU-Ni ibaada ya kushukuru,kushangilia, kumkubali,kumsifia,kumwadhimisha,na kumtukuza Mungu kwa matendo yake makuu aliyo,anayo na tunayoamini anaendelea kututendea.
Unaweza kumfanyia sifa kwa yale aliyoyatenda kwa wengine au hata ujumla wa matendo yake maishani mwetu!
*Mara nyingi imetafasirika kuwa sifa ni nyimbo za haraka na shangwe Ila natamani Mjue sifa zaidi ni maudhui na makusudi ya moyo wa mtaa sifa!!
KUABUDU-Ni ibaada ya unyenyekevu,heshima na adhama. Kwa Mungu kukubali,kutii na kumuadhimisha kwa sifa na tabia zake...Hapa haijalishi amefanya chochote kwako au hajajibu maombi yako kama uonavyo Ila anaabudiwa kwa JINSI ALIVYO!
Niweke msisitizo hapa yaani hata kama Huna kazi,umefeli au umeachika bado Yeye ni Mungu tu na Ni mtakatifu tu na Ni mwema tu!!!
*Pia kwa wengi imetafasirika kuwa kuabudu ni nyimbo za taratibu,za kulia na hisia kali...lakini Nataka Mjue kuwa kuabudu ni Maudhui na mwelekeo wa Moyo!!
Sasa Nani ni mwabudu halisi na Anayemsifu Mungu kweli???
Na imempasa nini mtu huyooo....??

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 2




Shalom!
..Nani mwabudu Mungu wa Kweli na imempasa kufanyaje???
LEO
Natamani kusisitiza mambo makubwa mawili tu katika sifa na kuabudu!!
Yaani haya yakae moyoni na kichwani mwa yeyote anayetamani kuugusa moyo wa Mungu kwa sifa na kuabudu,nayo ni haya;
1.LAZIMA KUMJUA NA KUMFAHAMU SANA HUYO MUNGU NA KUWA NA UHUSIANO NAYE.
Huwezi kufanya ibaada yeyote kwa Mungu ikawa ya maana kama unamsikia tu na humfahamu kabisa....imetupasa kumjua tena kumjua zaidi,tena kuwa na uhusiano naye wa karibu....maana kwa Kadri unavyomjua zaidi ndivyo unazidi kumpenda yeye na Kumsifu na kumuabudu kweli!....na hapo Ndio maandiko yanasema "Kusifu kwawapasa wanyofu wa mioyo"...Okey ngoja nitoe mfano huu,Kumsifu Mungu wakati hata hamna uhusiano wa karibu na sawa na kuona mjini gari aina ya Hammer ambayo iko mitaani kwenu na ukaanza kuwasimulia wenzio..."Oyaaa unaona ile hammer,yaani nyumba yetu hii unapita mtaa mmoja ndio nyumba ya mwenye gari ile aisee,yaani ile gari kali kishenzi yaani duh,Nyie Acheni tu mtaa wetu mambo Safi hahaha" sasa hapo wakikuuliza ni Tsh ngapi au umewahi kupanda au anakufahamu unabaki tu Aaah mmmm Oooh...Acha bwana hilo sio lenu, jivunie chenu...JIVUNIE MUNGU MAISHANI MWAKO,SIO KUMSIKIA TU!!
2.LAZIMA MUNGU PEKE YAKE NDIO AINUKE(AWE MAARUFU)
Yaani katika sifa na kuabudu usijitahidi kujiinua au kutaka kuonekana wewe au timu yenu au mchungaji wenu au Kanisa lenu Ila Mungu pekee Ndio wakuinuliwa!!
Kuna ukuta mwembamba sana kati ya kutafuta sifa na umaarufu au kujiona na unyenyekevu wa kutaka Mungu pekee Ndio aonekane!!
Tena sio kwa maigizo bali toka moyoni... Na ukiwa na moyo wa unyenyekevu utashangaa una Amani tele hata uende wapi au watu wawe kumi tu au vyombo visiwepo au sare zisiwepo hata usipopewa maji au nauli na popote ulipo kwa kuwa umeamua kumfanyia Mungu ibaada basi utashangaa sana udhihirisho wa nguvu za Mungu!!!
Tabia za kuonyeshana na watu ufundi wa Sauti au kucheza na kusahau kuwa malengo ni kumuabudu Bwana basi hapo ibaada yote huwa sifuri maana tumejitwalia utukufu machoni pa watu.
(Ila pia haimanishi pia kuwa sifa na kuabudu vinapaswa kufanyika ovyoovyo..ustadi unahitajika mno)
Mungu awasaidie sana wote mnaokaa mbele kuwaelekeza watu au kuwaongoza uweponi mwake ili Mjue hamfanyi kwa ajili yenu Ila.kwa ajili ya Mungu!!!
.....Je ladha ya Kusifu na kuabudu inatokana na.viungo gani???

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 3


Shalom ndugu yangu!
Naamini unaendelea vema na maisha yako na ninambariki Mungu sana kwa ajili yako na nimemwomba roho mtakatifu akusaidie kuendelea kuelewa somo hili!
Mara ya mwisho niliongelea mambo mawili makubwa kwanza ni Lazima Mtu anayetaka Kumsifu na.kumuabudu Mungu kweli lazima awe na uhusiano naye thabiti na pili katika sifa na kuabudu sio wewe au Kanisa au chochote kuinuliwa zaidi ya Mungu mwenyewe!
...Na nikaacha swali....JE NI VIUNGO VIPI HULETA UTAMU WA KUSIFU NA KUABUDU!!
Basi ninamshukuru sana Mungu kwa ajili yako na natamani niseme nawewe kwa habari ya uzuri wa sifa na kuabudu!
Sisi huwa tunadhani uzuri wa sifa ni Muziki(Melody),nyimbo tuzipendazo Sisi, mavazi yetu,mitetemeko ya waongoza sifa,machozi labda na mihemuko na hapo tunaweza kuruka na kucheza sana lakini hata kama Hayo yote huwepo au ni muhimu Ila msingi wa Utamu wa sifa na kuabudu ni haya yafuatayo;
1.Ibaada ya sifa na kuabudu yenye Utamu mbele za Mungu ni ile inayofanywa na Moyo wa kumpenda yeye,moyo Safi na wenye nia thabiti ya Kumsifu na Kumuabudu!!
2.Siyo nyimbo uzipendazo wewe ndio zinaleta utamu wa sifa mbele za Mungu,sio upendazo wewe maana sio kwa ajili yako Ila kwa ajili yake mwenyewe.... Ingawa ukizama sana utagundua kuwa kile roho mtakatifu anataka na wewe unaingiwa kupenda kile atakacho!!!
*Sasa natoa tahadhari tu.... Acha ubinafsi wa kutaka Kusifu na kuabudu kwa matakwa yako Ila msikilize sana roho ili mara zote umeona wingu lake!
3.Na tatu ni ile hamu ya kumtaka Mungu Atukuzike katika sifa na kuabudu ndio inafanya moyo wako uwe mnyenyekevu na kwa hakika Mungu ajidhihirishe na sio kuwa na hamu ya kutaka kusifiwa au kupongezwa baada ya uwepo kudhihihirika!
*Unajua Mungu akisifiwa hushuka lakini ile hamu yako ya kumuona Mungu zaidi na sio Kiasi wewe uonekane kama wewe ndio huwa unasifu na kuabudu mpaka uwepo unashuka!
4.Na mwisho;Ili ibaada ya Kusifu na kuabudu Iwe na tamu....Ni mara zote ikiwa unafanya ibaada ya sifa na kuabudu lazima uwepo umoja kati ya moyo wako au roho yako na nafsi yako na mwili wako lakini pia ikiwa mnafanya ibaada mkiwa wengi basi iwepo nia moja na mara zote muonekano wako, mkao wako na mavazi yako,yakupe nafasi ya kuwa na utulivu mbele za Mungu.... Haiwezekani ibaada ya sifa na kuabudu Iwe tamu wakati moyo na akili yako na nafsi yako havina ushirikiano....na huwezi kuwa huru kufanya chochote mbele za Mungu kama kucheza,kulia au kurukaruka hali mavazi yako yana thamani kuliko hiyo ibaada kiasi huwezi hata kupiga magoti,huwezi kucheza kwasababu ya hadhi au cheo chako au mavazi yako yanakubana au yanawakwaza wengine!!
Natamani roho mtakatifu akusaidie kuelewa haya,maana ibaada.ya sifa na.kuabudu ni ya Mungu mwenyewe na wakati wote kumbuka "ALITUUMBA ILI TUMUABUDU"
Basi wakati mwingine nitaendelea kuzungumzia kwa kina "Kwanini Sifa na kuabudu maishani mwetu? na nini uhusiano wake na makusudio ambayo Mungu alituumba nayo"

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 4


Shalom wana wa Mungu!

Wajoli na Wajeuri wa Bwana!
Tumekuwa na mfululizo wa kupendeza kuhusu sifa na kuabudu,na tangu tumeanza leo ni sehemu ya nne kati ya tano...na leo natamani kuzungumzia "Kwanini Sifa na kuabudu maishani mwetu" yaani muunganiko wa sifa na kuabudu na hatma za maisha yetu!
*Najua wengi tunajua Kusifu na kuabudu ni sehemu ya ibaada mbalimbali makanisani na ndio maana watu huanza kwa maombi,sijui matangazo kisha Kusifu na kuabudu, neno,sadaka na mengineyo Ila leo natamani nikujuze kuwa sifa na kuabudu ni zaidi ya hapo!!
Kusifu na kuabudu ni ibaada endelevu kila siku na kila mahali na kwa kila namna!
Ile ifanyikayo kanisani ni namna ya pamoja ya Kusifu na.kuabudu kwa upamoja na kwa utaratibu tuliojiwekea na kama watu wakibaki na picha hiyo pekee hawatafanya ibaada hiyo kwa ukamilifu!!! 

ZINGATIA UKWELI HUU!!
Kila mtu ameubwa kwa kusudi maalum hapa duniani na kila mtu amepewa uwezo fulani halisi unaomwezesha kufanya mambo yale yampasayo kwa urahisi kuliko yeyote mwingine(Yaani kwa mfano mimi sijitahidi kusheresha au kuchekesha maana ipo ndani naturally) na.uwezo huo huitwa kipaji na wazungu huongea kwa maringo zaidi "Gifts & Talents".....na kwa ujumla wake woote mambo haya ili tumwabudu Mungu!
Sasa kama tuna majukumu ya kufanya na hayo yote ni kwa ajili ya Kumwabudu Mungu na kuyafanya majukumu hayo ndio kuishi kwenyewe...tunaachaje kumwabudu Mungu??
Ile hali ya kujua kuwa hakuna jambo unaloweza kufanya kwa akili yako na uwezo wako binafsi na ule ukweli kuwa yote ufanyayo ni kwa utukufu wa Mungu....itakulazimu kuabudu tu,isipokuwa kama umeamua kuwa na Kiburi cha uzima na kujiona kama umejiumba mwenyewe!!
"Katika sifa Mungu hushuka" naamini umewahi kusikia sentensi hiyo Ila unadhani ni kwa ajili ya ile sifa ya kanisani pekee...Je hujawahi kusikia wale watu wa kale waliowahi kushinda vita kwa sifa?? Popote ambapo Yesu anasifiwa lazima uwepo wake uwe Kamilifu.... Sasa ukitaka mambo yako yaende sawia na kwa Ushindi lazima ukubali tu kujumlishia na Ibaada ya sifa na kuabudu!!

Kusifu na kuabudu ni kama vile kusema....MUNGU NI WEWE PEKE YAKO,HAYA YOTE NI YAKO,SHUKRANI TUKUZO NA SIFA ZOTE NI ZAKO,UMETUPA HIVI VYOTE KWA UTUKUFU WAKO,AHSANTE JEHOVA MAANA NI WEWE!!
Yaani kwamba sio kwa uwezo wako wala akili yako bali ni kwa Neema ya Mungu tu!!
Kusifu na kuabudu ni wakati wa shida na wakati wa raha,ukiwa na kusanyiko na hata ukiwa peke yako,ukiwa nyumbani na hata ukiwa mbali,kwa mavazi,muonekano, kelele, kula,kuongea,kufanya kazi na hata katika kujifurahisha!!
Muhimu kujua kuwa Umeumbwa ili umuabudu Mungu,utafundishwa kuwa mtumishi ama kuishi hatma yako au utafunzwa kuwa na ndoto au kuacha Alama itakayodumu ni sawa kabisa lakini msingi wa yote haya ni ili Mungu atukuzike..... Watu wamjue Mungu,waupokee Ufalme wake na wamuishi yeye....na hapo Ndio tunasema Maisha ya Ibaada,na.hiyo ibaada ndio Kusifu na Kumuabudu!!
Unaweza ukachoka Kumsifu alivyo mwema maishani mwako lakini kila uonapo watu wanakufa, wengine wanaumwa na hawa wapata shida....na hayo yawapatayo wenzio wewe huyashuhudii basi choka salama....na ukimjua Mungu sawasawa kuwa yeye hata nini kitokee duniani hakibadilishi Umungu wake...na kama ukijua ni baba yako,na AHADI zake kwako ni za milele,hutaacha kumuabudu leo kwasababu una mashida na machangamoto....Ila utamwabudu tu kwa kuwa yeye ni Mungu na tumaini lako la kesho maana ni hakika na Amina!
Mungu ni mwaminifu sana mara nyingine ni kiburi tu ndio huwa kinatufanya tumsifu na kumuabudu sana aitha tukiwa tuna vingi au tukiwa hatuna basi tunamlilia, na huo kwa hakika ni utoto!!
Basi Mungu akusaidie kuwa na maisha ya Kusifu na Kuabudu kila siku, kila wakati na kila mahali bila kujali nini wala nini na hakika uwepo wa Mungu hautapungua maishani mwako!!!
Kabla ya saa ile ya Agano nitamalizia sehemu ya tano na ya mwisho kwa habari ya mambo makubwa mawili;
i. Namna ambazo unaweza kufanya ibaada ya sifa na kuabudu
ii. Mambo yakupasayo kuzingatia uwapo mstari wa mbele katika kuwaongoza wengine katika sifa na kuabudu!!
Ahsante Bwana Yesu kwa kila asomaye na kuelewa somo hili,lisaidie Kanisa lijue kina na msingi wa Ibaada kuwa ni SIFA NA KUABUDU....maana hata Malaika, maserafi, makerubi,wazee 24,wenye uhai wa nne na Sisi watakatifu tuliyo duniani na hata saa ile ya mwisho kule mbinguni biashara ni moja tu "KUMSIFU NA KUMWABUDU MUNGU"

KUHUSU KUSIFU NA KUABUDU-Sehemu ya 5(mwisho)


Shalom!
Yesu Kristo asifiwe sana!
Naamini uliyekuwa unafuatilia mfululizo huu umejifunza mengi na kubarikiwa pia,leo katika sehemu ya tano...Kuhusu kusifu na kuabudu, kama nilivyoahidi sehemu ya nne,tutaangazia mambo mawili makubwa;

I.NAMNA UNAVYOWEZA KUFANYA IBAADA YA SIFA NA KUABUDU!!
Kumfanyia Bwana ibaada,inategemeana sana na mahusiano yenu...yaani ningeweza kuwianisha na Mama na mwanae,namna ya kumlisha inategemea sana na urahisi wa mtoto huyo kula na kushiba, mwingine hula akipakatwa,mwingine hula akiwa anaoga, mwingine akiwa peke yake,muhimu ni kuwa mtoto amekula!!
Ibaada njema ni ile inayoanzia ndani ya kilindi cha moyo kabisa kwa upendo mkubwa,hivyo unaweza kufanya ibaada hiyo kwa namna nyingi,na hizi ni chache ambazo zimewahi kutumika na watumishi mbalimbali katika Biblia!
Unaweza Kumsifu na Kumwabudu Bwana:
1.Kwa kuimba,Iwe kanisani au popote pale-na hapa inaweza kuwa nyimbo za vitabuni, tenzi au zaburi au nyimbo mpya za kutoka moyoni mwako unapotafakari ukuu wa Mungu!
2.Kwa kupiga kelele-hii inaweza kuwa kelele zisizo na mpangilio au vigelege au miluzi au kelele zenye mpangilio wa nyimbo fulani!
3.Kwa kucheza -furaha ya mdundo unaoanzia ndani na sio ilimradi tu kuna muziki,na kwa habari ya kucheza unaweza kucheza hata kama hakuna muziki wowote
4.Kwa ubunifu na kazi za sanaa-mfano uchongaji,uchoraji, uigizaji na kazi nyingine za sanaa ambazo mwisho wa siku Ni Mungu ndio anasifiwa na kuabudiwa peke yake
5.Kwa kulala -unaweza ukalala namna yeyote ile kama ishara ya kujinyenyekesha mbele za Bwana
6.Kwa kupiga magoti
7.Kwa kukaa kimya mbele za Bwana
8.Kwa Kulia
9.Kwa kucheka
10.Kwa kunena kwa lugha nyingine,ziwe za duniani au lugha za kimbinguni!
11.Kwa kuomba
.....Sasa sifa na kuabudu inawiana na kuingiliana sana na maombi japo unaweza Kumsifu na Kumwabudu Bwana kwa maombi!!
Hizo ni chache katika namna nyingi,ambazo unaweza kujidhihirisha mbele za Bwana!!
Watu wengi wamechukuliwa na sifa na kuabudu ile ya kuimba na kucheza labda na kulia kanisani kwa maombi,na ni sawa tu!
Ila jambo la pili ni

II.NAMNA IMPASAVYO KUWA YEYOTE AKAAYE MBELE KUONGOZA WENGINE KATIKA IBAADA YA SIFA NA KUABUDU!
Wengi hufanya kama mazoea au utaratibu tu wa ibaada kwasababu wameshaguliwa au wamefanya mazoezi au wanajua au wana vipaji lakini ni zaidi ya hapo,imekupasa. Kuwa moyo mnyofu na Ibaada nzuri huanzia ndani yako kwanza kabla wengine hawajapotelea katika wingu,
1.Imempasa mtu huyu kuwa mtakatifu/mtauwa na anayempenda Mungu kiasi cha kupenda kumfamyia ibaada hata akiwa peke yake kabla hata kuwa mbele za watu
2.Imempasa kuwa na Neno la kutosha moyoni mwake,sio maandiko ya kukariri
3.Imempasa kuwa mwombaji, maana imempasa kusikia sauti ya Mungu wazi wazi ili awapo madhabahuni asifanye kwa mazoea
4.Imempasa kuwa na muonekano usioleta maswali kwa watu,yaani mavazi,mapambo na hata kutembea tu.
5.Imempasa kuwa na Amani na watu maana ikiwa mtu huyo ana Ugomvi au maneno maneno na watu,ibaada hiyo haiwezi kukamilika
6.Uongo,uzinzi,Umbeya, Unafiki na udhalimu wowote ule usitajwe kwake akaaye mbele za watu!...maana sifa na kuabudu kwa mwenye dhambi ni kelele mbele za Mungu!
7.Imempasa kuwa mnyenyekevu na aliye jaa hekima,na asiyejaribu kujitutumua au kujiona ni yeye na.bila yeye uwepo ule usingeshuka!
Lazima umaarufu, vyeo,elimu na hadhi viwe chini ya Utukufu wa Mungu,hivyo yeyote akaaye mbele za watu ajue kabisa kuwa yuko hapo kwa ajili ya Kumsifu na Kumuabudu Mungu tu na sio kuonekana!!
Mungu Roho mtakatifu akusaidie sote kuelewa sana zaidi ya maandishi haya,ili ibaada zetu za sifa na kuabudu, ikiwa ni za binafsi au mbele ya watu zipate kibali mbele za Mungu!
Mungu akuwezeshe na Mungu akunyenyekeshe ewe Mwabudu!!
Mpaka hapa Nimemaliza kwa habari ya Kusifu na kuabudu na ninayaacha kwako wewe kujifunza na kufundisha na kushare na wengine pia!!
*Najua utakuwa unajiuliza mbona hamna mistari ya Biblia,ndio! sitaki watu wanaokariri Nataka wanaoelewa!!!
Mungu akubariki sana wewe rafiki yangu!!
*Karibu sana katika Ulimwengu wa Kusifu na Kuabudu,kwa roho na kwa akili kwa kupenda!!

***MWISHO***
(c)King Chavvah, 2014
+255 713 883 797

KUSHINDANIA IMANI.

Historia imejaa simulizi ya watu waliotetea na kushindania imani zao dhidi ya upinzani.
Wapenzi nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari za wokovu ambao ni wetu sisi sote, Naliona imenilazimu kuwaandikia, ili mwonyane kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu waliondikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Yuda 1:3
Yuda anawatia moyo watu wa Mungu kusimama kidete dhidi ya ukengeufu wa nyakati zake na kuitetea imani ya kweli. Watu wenye hila waliingiza mafundisho ya uongo katika kanisa ili kupotosha imani. Inashangaza leo jinsi watu wengi wanavyojitoa kufuata na kutetea imani kengeufu na mafundisho mapotofu kuishi. Haki za mashoga, imani za waganga wa kieneyeji, kujitoa mhanga kwa kujilipua ili kutimiza jihad, maafundisho ya dini mfu zisizo na msaada kwa roho za watu zinasisitiza taratibu za nje kama kubatizwa, kuzikwa na kiongozi wa dini na sherehe mbali mbali za dini bila mabadiliko ya kweli moyoni .
Yuda anatuhimiza kuweka nguvu zetu katika imani sahihi inayoleta wokovu toka kwa kwa Bwana Yesu. Wokovu ni maisha ya imani yanayoegemea kwa Bwana Yesu na kuongozwa naye. Ni maisha ambayo Yesu Kristo ndio mhimili, maana yake ni mwokozi. Hivyo jina Yesu linaisimamia kazi aliyokuja kufanya hapa duniani. Kama vile Mkulima ni jina la kazi afanyayo mtu anayefukua ardhi na kupanda mbengu na kuzitunza hadi kuvuna mazao, kama vile mwalimu kazi yake ni kufundisha basi mwokozi kazi yake ni kuokoa. Na kwa vile alikuja hapa ulimwenguni ina maana Mungu alipenda wokovu utufikie hapa duniani. Nikisema nimeokoka maana yake Mwokozi Yesu ametenda kazi katika maisha yangu. Yesu asipookoa basi hastahili kuitwa Yesu (Mwokozi)
IMANI KATIKA YESU KRISTO NI MUHIMU SANA.
Tunaweka msisitizo mkubwa katika imani ya wokovu kwa sababu kulingana na 1 Pet 1:6 imani ya wokovu ina thamani sana. Thamani yake inathibitishwa na vipimo vya ubora ambavyo ni majaribu. Imani ya wokovu inavuka majaribuni bila kumwaibisha mwokozi. Kama dhahabu inavyopimwa kwa moto, majaribu pia huipima imani ya wokovu na kuithibitisha.
• Hii ni imani takatifu Yuda 1:20 Imani ya wokovu imebeba upekee wa Mungu. Sifa ya uaminifu, ukweli na haki. Haichanganyi uongo au hila au ukatili katika kumwabudu na mkumfuata Yesu. Imebeba upendo na huruma, uaminfu na usafi. Imani ya wokovu haikubaliani na maisha ya uovu.
• Inatolewa mara moja Yuda 1:3 Biblia hudai Kristo baada ya toleo moja dhidi ya dhambi ameketi (amepumzika).
Waebrania 10:12,26, 33-34 Samson alitengeneza na kujirudi kabisa lakini alipoteza maisha yake pamoja na kisasi cha Wafilisti. Ni vigumu sana kurudi pale ulipokwishafikia na Bwana, gharama yake ni kubwa kurudi mahali uliokuwa kwanza.
Esau alitafuta sana nafasi ya kutubu hakuipata, Yakobo akachukua nafasi yake, naye Yuda Iskariote hakupata tana ile fursa aliyopoteza na usimamizi wake akautwaa mwingine.  
LEO TUNAITWA KUSHINDANIA IMANI KWA SABABU:
1. NI NGAO YA MTU WA MUNGU. Usalama wa mtu Mungu umesimama hapo. Efeso 6:16 Shetani akitaka kudhuru mtu anawinda ngao yake ili kumwondolea ulinzi. Bila ulinzi huna kinga maana kila shambulio litakupata (UKOSEFU WA KINGA YA KIROHO)
2. NDIO MKONO WA KUPOKELEA MEMA NA BARAKA TOKA KWA BWANA Yakobo 1:6,7 Marko 11:24
3. NDIO NJIA (MAISHA YA MTU WA MUNGU) Hatuenedi kwa kuona 2 Wakolosai 5:7
4. NDIYO NJIA PEKEE YA KUMPENDEZA MUNGU. Waebrania 11:6 hapa inaelezwa mfano wa Maisha ya Henoko. Huu ni mfano mzuri wa mtu aliyeishi maisha ya kumpendeza Mungu. Bwana akaenda naye. Wako wapi watakaoenda na Bwana katika nyakati zetu. IKIWA UNATAKA KWENDA NA BWANA KATIKA MAISHA YAKO ITABIDI USHINDANIE IMANI YAKO. Jiunge na watumishi wa Mungu wa nyakati zote kuitetea imani yako.
KUNA ORODHA NDEFU YA MASHUJAA WA IMANI.
Naambiwa Mathayo alitetea imani yake na wokovu hadi akauwa kwa upanga kule Ethiopia.
Marko naye katika kuihubiri imani ya wokovu aliuawa pale Alexandria Misri baada ya kuvutwa na magari ya farasi katika njia za mji.
Luka yule tabibu naye alisimama kidete kwa imani yake hadi akatundikwa katika mti wa mtende pale Ugiriki.
Yohana naye baada ya kushindikana kumwua kwa kumtupa katika mafuta yanayochemka alifungwa katika kisiwa cha Patmos.
Petro alipotishiwa kusulubiwa asipoikana imani ya wokovu aliomba asisulubiwe kama Yesu badala yake yeye awekwe kichwa chini miguu juu. Akauwa kule Roma akiitetea imani yake kwa Yesu.
Yakobo alikatwa kichwa Yerusalem lakini hakuikana imani yake.
Bathlomayo alichunwa ngozi katika mateso ya kujaribu kumfanya aikane imani.
Andrea alikusulubiwa msalabani akiwahubiri waliomsulubu juu ya uzuri wa Bwana Yesu hadi akafa.
Thomas akihubiri imani ya wokovu kule India alichomwa mikuki kule India hadi akafa.
Yuda alipigwa mishale na kufa bila kuikana imani yake,
Mathia alipigwa kwa mawe kisha akakatwa kichwa bila kuikana imani yake.
Barnaba aliuawa kwa kupigwa mawe kule Salonike na,
Paulo akakatwa kichwa na Nero kule Roma, wote hawa wakabaki wakitetea imani yao kwa Yesu.
Mimi pia sikuwahi kupata upinzani kuhusiana na imani hadi nilipookoka.
Paulo vile vile ndipo akasema “wote wapendao maisha ya utauwa wataudhiwa” 2Tim 3:12
HATUWEZI KUIKIMBIA HISTORIA, WALA HATUWEZI KUMBADILI MUNGU AU SHETANI. TUNAWEZA KUBADILIKA SISI.
Ikiwa tutasimama kuitetea imani yetu, ndipo itakapodhihirika kuwa imani yetu ina thamani na ubora wake kufunuliwa.
Mungu akubariki

....****MWISHO****....



UCHUMI WA UFALME WA MBINGUNI                            


   Mama mmoja aliyekuwa na watoto sita (lakini alikuwa hajaolewa), alipelekwa na mwenzake kwa Askofu wa dhehebu lao ili wapate msaada kwa kuwa walikuwa na maisha ya shida sana. Yule mama pamoja na watoto wake sita walikuwa wanakaa katika nyumba ya makaratasi, na hawakuwa na chakula cha kutosha.

Askofu alimuuliza yule mama amewapateje wale watoto wote sita na huku alikuwa hajaolewa.
Yule mama akajibu akasema; "Mtoto wa kwanza nilimpata kwa kuwa nilikuwa nataka mtoto, niliona nazeeka bila ya kuolewa nikaona nizae mtoto, Lakini mtoto wa pili nilimpata wakati nilipokuwa natafuta chakula cha mtoto wa kwanza. Mtoto wa tatu nilimpata nilipokuwa natafuta chakula cha watoto wawili niliokuwa nao. Na hali hii imeendelea mpaka sasa nina watoto sita – na sijui nitaendelea na hali hii mpaka lini".
Ni wazi kabisa si mapenzi ya Mungu huyu mama aishi maisha ya namna hiyo. Vikwazo vya uchumi ambavyo vilimzunguka yule mama na watoto wake vilitoka kwa ibilisi.
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ……."(Hosea 4:6). Maneno haya yaliyosemwa na Mungu kwa kinywa cha Nabii Hosea yana ukweli ndani yake hata hivi leo. Watu wengi sana siku hizi wanaangamizwa, wanadhulumiwa, wanahuzunishwa na maisha kwa sababu tu wamekosa kuyajua maarifa ya Mungu yaliyomo katika Neno lake.
Wakati fulani nilikuwa nafundisha katika semina moja juu ya uhusiano wa maendeleo ya mtu na Wokovu, na wakati wa kipindi cha majadiliano Mchungaji mmoja akatueleza habari iliyotufikirisha sana.


Akasema ya kuwa katika kanisa alilokuwa analihudumia miaka ya nyuma aliwahi kufuatwa na mama mmoja wa usharika huo ambaye alikisema ya kuwa yeye alikuwa mmoja wa wakina mama thelathini ambao hawashiriki chakula cha Bwana kwa kuwa walikuwa wanaishi hapo mjini kwa njia za umalaya. Ombi lao kwa mchungaji wao lilikuwa ni kwamba akiweza kuwasaidia kupata kazi za halali waache umalaya. Wao wametafuta kazi bila ya mafanikio, na wanafanya umalaya si kwa sababu wanapenda, bali kwa kuwa hawakuwa na njia nyingine ya kupatia fedha.
Ni jambo la kumshukuru Mungu, ya kuwa mchungaji yule aliweza kuwatafutia kazi wale wakina mama wote katika kiwanda kimoja, na maisha yao yakabadilika wakaacha umalaya, na kuishi maisha ya kikristo yenye ushuhuda.
Ni watu wangapi ambo wanaishi maisha yao kinyume na maadili ya kikristo ili kupata fedha za kuwasaidia kila siku? – Ni wazi kuwa ni wengi. Je! hawawezi wakapata riziki yao bila kudhulumu au kuiba au kudanganya au kuzini? – Ni wazi kuwa wanaweza. Sasa, ni kwa nini wanaishi kwa jinsi hiyo?
Jambo ambalo watu wanahitaji kujua ni kuwa baba wa uongo yaani shetani amewadanganya kwenye mawazo ya kuwa hakuna njia nyingine ya halali ya kupatia fedha isipokuwa hizo. Na shetani anausimamia uongo huo ili uonekane kuwa ni kweli kwa kuwawekea watu hasa wakristo vikwazo vigumu vya kiuchumi.
Unaweza ukawa unajiuliza vikwazo hivyo ni vipi? Vikwazo hivi vinatofautiana katika watu mbalimbali na mahali mbalimbali. Kuna watu wengine wataona hakuna mradi wa halali wanaoufanya unaofanikiwa. Mwingine miradi yake inafanikiwa, lakini fedha yote inaishia kutafutia matibabu ya magonjwa yaliyomo ndani ya nyumba yake ambayo hayaishi.
Mwingine anapata magari mengi, lakini hayaishi kupata pancha na kuharibika au kuanguka. Mara nyingi utawasikia watu wa jinsi hii wanasema wana mkosi. Kwa kweli si mkosi bali vikwazo vya kiuchumi toka kwa shetani ili ushindwe maisha na UANZE KUTAFUTA MAISHA MAZURI KWA NJIA ZILIZO KINYUME NA MAADILI YA KIKRISTO YALIYO MATAKATIFU.
 

Jambo ambalo wakristo wengi hawalifahamu
 Mimi na mke wangu miaka ya mwanzo tulipookoka hasa mwaka 1984 na 1985 tulikumbana na vikwazo vigumu sana vya kiuchumi. Tuliona jinsi maisha yalivyokuwa yanarudi nyuma – fedha tuliishiwa, chakula tuliishiwa, nguo tuliishiwa, vitu ndani vilianza kuharibika na hatukuwa na fedha za kuvitengenezea. Tulijaribu kulima bustani za mboga, hazikufanikiwa. Tulijaribu kupika chapati za kuuza, hazikununuliwa zikaharibika tukazitupa.
Kwa kifupi tuliona maisha ya wokovu kuwa ni magumu, ya shida na ya kimaskini sana. Tulishindwa hata namna ya kuwasaidia ndugu zetu vizuri. Hali hii ilitutia uchungu sana. Watu hawakufahamu ya kuwa hali hii ilikuwa inatunyima amani ya kweli ya wokovu – kwa kuwa tulijitahidi kuwachangamkia wote ili kuficha mapambano tuliyokuwa nayo kimaisha.
Ilikuwa ni vigumu sana kuishi maisha ya ushuhuda mzuri wa kikristo katikati ya mahitaji makubwa kama hayo tuliyokuwa nayo.
Tulijua kuwa Zaburi 23:1 inasema, "Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu". Lakini tulikuwa tumepungukiwa na vitu vingi vya lazima katika maisha. Hatukufahamu kwa nini sisi kama kondoo wa Kristo tulikuwa tumepungukiwa namna hiyo!
Tulikuwa tunasoma lakini tunashindwa kumwelewa Mtume Paulo alipokuwa anasema katika Wafilipi 4:12 kuwa; "najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa".
Tuliona ya kuwa Mtume Paulo aliweza kuwa na amani na ushindi katika hali yo yote aliyokuwa nayo – hata katika upungufu. Sisi tulikosa amani tulipokuwa tumepungukiwa! Na hili jambo lilitusumbua sana.
Tulikuwa tunafurahi tunaposoma mstari kama ufuatao; " …..vyote ni vyenu …. Vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu, nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu"(Wakorintho 3:21,22). Tulikuwa tunafurahi kwa kuwa maneno haya yanatupa uhalali wa kumiliki vitu vilivyo vya Mungu. Kwa mfano Hagai 2:8 inasema "Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa Majeshi." Pia, Zaburi 24:1 inasema "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana …" Lakini jambo lililotusumbua ni kwamba ingawa mistari hiyo ilitupa umilikaji juu ya fedha, dhahabu na vyote viijazavyo nchi ili tuvitumie – SISI HATUKUWA NAVYO WALA HATUKUJUA TUTAVIPATAJE!
Tulifahamu ya kuwa ni mapenzi ya Mungu tufanikiwe katika mahitaji ya kiroho na mahitaji ya mavazi, chakula, na malazi; soma kitabu cha 3 Yohana 1:2. Kwa hiyo tulikuwa na hamu kubwa ya kufanikiwa.
Tulitamani sana kuona maneno ya Wafilipi 4:19 yanatimia kwetu – nayo yanasema hivi;
"Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu".Hali hii ilitufanya tuingie katika maombi mazito, ili kumuuliza Mungu njia na namna ya kuondokana na hali tuliyokuwa nayo.
Mambo makubwa matatu yafuatayo, Roho wa Mungu alituambia kuwa ni chanzo cha matatizo yaliyokuwa yanatukabili: Alituambia yafuatayo:
Kuwa, ingawa tumezaliwa mara ya pili na kuingizwa katika ufalme wa Mungu – tulikuwa bado tunategemea utaratibu wa uchumi wa duniani badala ya kutumia na kutegemea utaratibu wa uchumi wa mbinguni;
Kuwa, tulikuwa tunapenda kupokea bila ya kuwa watoaji, na pia tulitaka kuvuna tusichokipanda. Roho Mtakatifu aliuliza swali, Je! unaweza kwenda kwenye bustani yako kuchuma nyanya huku ukijua kuwa hujawahi kupanda nyanya? Ni wazi kuwa jibu lilikuwa ni hapana.
Kuwa, hatujafahamu ya kuwa adui yetu ibilisi ndiye chanzo cha mahangaiko na mafadhaiko yaliyoambatana na kupungukiwa mahitaji katika maisha. Na pia tulikuwa hatutumii silaha tulizopewa ili kuzivunja kazi za ibilisi katika maisha yetu.
Baada ya kupokea majibu hayo kutoka kwa Mungu, tulitubu na kuomba msamaha. Tuliendelea kumwomba Mungu atufundishe na atuongoze katika kuishi maisha ya kutumia na kutegemea utaratibu wa uchumi wa ufalme wa mbinguni.
Mafundisho tuliyoyapata yalituondoa katika mahangaiko ya kupungukiwa na kutuingiza katika furaha na amani ya mafanikio NDANI YA KRISTO.
Ndiyo maana tumechukua hatua hii chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu kukushirikisha baadhi ya mafundisho hayo ili ikiwa umo katika hali ya mahangaiko ya kupungukiwa na mahitaji muhimu ya maisha upate msaada wa kuondokana nayo.
Kumbuka ni mapenzi ya Mungu ndani ya Kristo kuwa ufanikiwe na uishi maisha ya ushindi katika maeneo yote ya maisha yako na katika siku zote utakazoishi juu ya nchi.
 

Mwenye haki ataishi kwa imani
 Nabii Habakuki aliishi katika kipindi kilichokuwa kigumu sana kiuchumi. Hali hii iliwafanya watu wengi kuingia katika dhuluma, udanganyifu na mambo mengine maovu ili tu waweze kuishi.
Lakini kilichoumiza moyo wa Nabii Habakuki ni kuona kuwa kulikuwa na watu wachache ambao hawakufuata mambo maovu – lakini waliishi maisha magumu na kuonewa na matajiri wa wakati huo. Hali hii ilimfanya Nabii Habakuki aingie katika maombi ya kumlalamikia Mungu, huku akihitaji kujua mpango wa Mungu juu ya watu waliosimama upande wake. Soma kitabu cha Habakuki sura ya 1 na 2.
Kati ya jibu ambalo Mungu alimpa Nabii Habakuki juu ya maisha ya watu wake katikati ya hali ngumu ya uchumi ni maneno haya;
"….mwenye haki ataishi kwa imani yake" (Habakuki 2:4)
Huu ndio uliokuwa mpango wake kwa watu wake wakati ule ili uwasaidie kuishi katikati ya dhuluma na maovu yanayotokana na hali ngumu ya uchumi.
Katika siku hizi za mwisho, kumetabiriwa kutokea tena hali ngumu ya uchumi inayoambatana na dhuluma pamoja na maovu mbalimbali. Mungu amekwisha andaa mpango mzuri kwa ajili ya wote watakaoipokea na kuikiri injili ya Kristo inayookoa. Na mpango huu ni sawa na ule aliopewa Nabii Habakuki.
Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Mtume Paulo alisema maneno muhimu yafuatayo:
" Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa , MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI" (Warumi 1:16-17). Huu ndio mpango wa Mungu kwa watu wote wanoipokea Injili ya Kristo na kuokolewa. Katikati ya dhuluma,wizi, uasherati na maovu mbalimbali yanayoambatana na hali ngumu ya uchumi iliyopo sasa na ile itakayotokea miaka si mingi iliyo mbele yetu kuanzia sasa – Mungu anawataka watu waishi kwa kufuata mpango wake – WAISHI KWA IMANI.
Kuishi kwa Imani ndiyo utaratibu wa uchumi wa mbinguni ambao kila mkristo anatakiwa kuufuata akitaka kuishi maisha ya mafanikio na matakatifu katikati ya hali ngumu ya uchumi – badala ya kujikuta amewezwa na masumbufu ya maisha haya.
Inasikitisha kuona kuwa wakristo wengi wameyatafsiri na kuyatumia vibaya maneno haya "kuishi kwa Imani". Na kwa ajili hiyo mpango wa Mungu uliomo ndani ya maneno haya haujaeleweka na wengi.
Wakristo wengine wanafikiri kuishi kwa imani ni kuacha kazi wanazozifanya na kuanza kuishi maisha ya omba omba na ya kubahatisha. Wamesahau kuwa biblia inasema mtu asipofanya kazi asile – soma 2Wathesalonike 3:6 – 12.
Ingawa kuna wakristo ambao wamelifanya neno hili "kuishi kwa Imani" lisieleweke vizuri; hali hii haiwezi wala haitaweza kubadilisha mpango wa Mungu uliomo ndani yake.
Mawazo yetu siyo mawazo ya Mungu; njia zetu si njia za Mungu; na mipango yetu si mipango ya Mungu. Hakuna njia ya mkato kwa mkristo safi ya kufanikiwa katika maisha, isipokuwa ni kwa kuishi ndani ya mpango wa Mungu uliofunuliwa katika Kristo Yesu.
"Mwenye haki ataishi kwa imani" maana yake nini? "Mwenye haki" maana yake Mkristo, au Mtakatifu, au Mwongofu, au Mteule, au Aliyeokoka. Kwa hiyo tunaweza kusema Mkristo ataishi kwa imani.
Pia tunasoma katika Waebrania 11:1 ya kuwa:"Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana"
Tena imeandikwa katika Warumi 10:17 ya kuwa;"Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo".
Tena imeandikwa katika Yakobo 2:26 ya kuwa;"Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa".
Kwa mistari hiyo michache na mingine mingi iliyomo katika Biblia inatusaidia kujua ya kuwa "Mwenye haki ataishi kwa imani"maana yake kila mkristo anatakiwa kuishi kwa kuwa mtendaji wa Neno la Kristo na siyo msikiaji tu – kila wakati na katika kila eneo la maisha yake.
Roho Mtakatifu alipokuwa anatufundisha haya mimi na mke wangu, tulijua hakika ya kuwa tunatakiwa kutumia muda mwingi kulisoma na kulitafakari Neno la Kristo, ili tuweze kulitenda Neno hilo katika maisha haya. Tulianza kusoma Neno la Mungu na vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na watumishi wa Mungu na bado tunaendelea kufanya hivi hata leo, na tumeona mabadiliko makubwa katika maisha yetu – maana mahangaiko tuliyokuwa nayo yametoweka kwa jina la Yesu Kristo! Sasa tunaishi katika maisha ya ushindi na amani ndani yake Kristo.
Tatizo ambalo mtu analipata anapookoka, ni namna ya kuishi katika maisha mapya ya wokovu (2Wakorintho 5:17)
Biblia inatuambia ya kuwa sisi ni raia wa nyumbani mwake Mungu (Waefeso 2:19). Pia inatuambia kuwa sisi si wa ulimwengu huu (Yohana 17:14). Kwa hiyo maisha yetu hayatakiwi kuongozwa na utaratibu wa hapa duniani.
Kuna tofauti kati ya utaratibu wa uchumi wa duniani na utaratibu wa uchumi wa ufalme wa mbinguni. Ingawa sisi tulio wake Kristo tumo humu ulimwenguni hatutakiwi kuishi kwa kutegemea utaratibu wa uchumi wa dunia hii unaoyumba, bali tutegemee utaratibu wa uchumi wa ufalme wa mbinguni – usioyumba wala kubadilikabadilika kwa kuwa umejengwa juu ya mwamba imara – Neno la Kristo.
Wakristo wengi kwa kutokujua hili wamejikuta wakipata shida ya kutaka kuwatumikia mabwana wawili – yaani Mungu na Mali ambapo Yesu Kristo alikwishasema haiwezekani. Matokeo yake ni kupoteza ushuhuda wa kikristo na kuishi maisha ya mahangaiko.
Kutegemea utaratibu wa uchumi wa dunia hii kuna shida sana kwa kuwa uchumi huo ukiyumba kidogo, na wewe unayumba kimaisha. Lakini ukiutegemea utaratibu wa uchumi wa ufalme wa mbinguni huwezi kuyumba wakati uchumi wa dunia ukiyumba – kwa kuwa tumaini lako halimo mikononi mwa dunia na wanadamu – bali ndani ya Kristo Yesu ambaye ni mwamba imara usiotikisika.

Mwl. Mwakasege

( IMETOLEWA -INJILI YA YESU KRISTO TANZANIA)

....****MWISHO****....
       

No comments: