Kanuni

UHALISI  WA NENO'' UKWATA''
UKWATA-Ushirika wa Kikristo wa  Wanafunzi   Tanzania au kwa kiingereza (TSCF)
yaani '' Tanzania students christian   Fellowship''

MISINGI  YA IMANI  YA CCT-UKWATA

(a) Wanachuo  wa ushirika  wa wakikristo  wa wanafunzi  Tanzania tunamkubari YESU KRISTO KUWA NI MWOKOZI NA BWANA  wa watu  wote  wanaomwamini
(b) Tunaamini  katika  utatu Mtakatifu  yaani   Baba.Mwana  na  Roho   Mtakatifu.
(c) Tunaamini  kuwa maandiko matakatifu yaani Biblia   kuwa ni Neno  la  Mungu
 ambalo  lina misingi  ya  kweli  iliyo  ya muhimu kwa maisha  na wokovu wetu na kukiri imani ya mitume


MALENGO  AU  MADHUMUNI  YA  CCT-UKWATA

(a)  Kuwasaidia  wanafunzi  wampokee  YESU  KRISTO   kuwa  mwokozi  na Bwana wa maisha yao na waishi kwa kufuata kukubali kwao,wakishuhudia,wakitangaza  habari  njema na kutumika katika nchi yao na ulimwengu wote
(b)  Kuwaelea  wanafunzi/wanachuo katika msingi wa maishaya Kiroho  kwanjia ya ibada  ya  pamoja  kujifunza   Biblia na Sala
(c) Kujenga  moyo kufuata tabia ya YESU KRISTO  kwa wanafunzi/wanachuo   katika kuwahudumia
  watu  wenye  matatizo ya kimwili na Kiroho nchini na ulimwenguni mwote
(d)  Kuwatia moyo wanafunzi /wanachuo  katika kufikiria  juu ya wito wa  kulitumiikia  kanisa na kukuza mwelekeo  wa  kanisa na jamii
(e)  Kukuza  maarifa  katika  maandiko  matakatifu(Biblia) na karama  za Rohoni


SIFA ZA  MWANACHAMA  WA  CCT-UKWATA
(a)Mwanachuo anayetoka  katika kanisa  lililo  mwanachama  wa jumuiya ya Kikristo
Tanzania(CCT) ikiwa:-
                  (i) Atakubaliana  na  katiba ya CCT-UKWATA  na  kulipa kiingilio  atapewa  kadi   ya
                     uanachama
                   (ii )Atalipa  ADA  ya mwaka,michango na kuhudhuria shughuli zinazopangwa  na 
                        wana UKWATA wenyewe  kwa  uaminifu
(b) Kwa mwanachuo  anayetoka katika  makanisa yasiyochini  ya CCT lazima  akubali  na kuwa na sifa zilizotajwa  hapo  juu  kwa utii wa Mungu.
(c )Mwana CCT-UKWATA lazima ahudhurie  shughuli,vipindi vya ibada  na kutii ratiba inayopangwa kwa uaminifu.
(d) Mwana CCT-UKWATA hai lazima awe na ushuhuda unaomtambulisha YESU KRISTO kwa ukamilifu  bila kuchafua vazi lake kwa ushuhuda mbovu.
(e) Mwana CCT-UKWATA lazima akubali   kuwa ni kiungo cha UKWATA na atumike kwa kujituma bila kulazimishwa kwa moyo wake kiutendaji.



MWANA CCT-UKWATA  ATAPOTEZA UANACHAMA  WAKE  ENDAPO:-

(i) Atashindwa  kutimiza katiba  ya CCT-UKWATA na taratibu  zote zilizowekwa kwa uaminifu
(ii) Atakosa ushuhuda mzuri wa kikristo,katika CCT-UKWATA,Taasisi aliyomo na katika jamii.
(iii) Mwana CCT-UKWATA Mshirikishwa  atapoteza uanachama  wake endapo atashindwa kutimiza katiba ya CCT-UKWATA.

KUPATA CHETI
(i) Kila mwanachama anahaki ya kupata cheti cha UKWATA kama ametimiza masharti na kuifuata katiba.
(ii) Mwanachama atakosa cheti kama atakosa sifa za uanachama kama ilivyotajwa hapo juu bila kuvunja hata moja.
(iii) Katika kutooa vyeti kila mwaka kutakuwa na mahafali moja tu ya kuwaaga wahitimu wa fani zote
ambayo itapangwa na viongozi wa  tawi.

            WAEBRANIA 10:25
   Wala tusiache kukusanyika pamoja  kama ilivyodesturi
  ya wengine  na kuzidi kufanya hivyo  kwa kadri            mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.  


BWANA  YESU  AWABARIKI  .

No comments: