JE, WAJUA YALIYOJIRI KATIKA BONANZA.......?

       Mnamo tarehe 13/12/2014 katika viwanja vya seminari vinavyopatikana ndani ya chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), kulikuwa na bonanza lililohusisha wanafunzi wa chuo kikuu cha kikatoriki cha Sayansi na Tiba Bugando na wale wa SAUT wote wakiwa ni kutoka kikundi cha USCF.

     Mashindano yalifunguliwa na mbio za wenyeviti, na Mwenyekiti wa Bugando aliwakilisha vyema kwa kuibuka mshindi wakati Mwenyekiti msaidizi wa SAUT nae aliibuka mshindi.

     SAUT waliweza kuibuka washindi katika mashindano ya kuijua vyema Biblia, mashindano ya kula, na kuvuta kamba.

     Wakati Bugando wakiibuka vinara katika mbio za mita mia, mbio za kupokezana vijiti,   kukimbiza kuku,pamoja na  kutembea na chupa kichwani

     Mchezo wa mpira wa miguu kwa wakaka, SAUT waliibuka washindi kwa kushinda goli tatu wakati Bugando wakishindwa kujitetea. (SAUT 3 - 1 Bugando).

    Mpira wa pete kwa wadada, SAUT walichakazwa na Bugando kwa magoli 13 kwa 1. (Bugando 13 - 1 SAUT).

    Lakini pia ipo michezo ambayo ilibidi pointi zigawanywe kwa wote, ambapo kukimbia kwenye magunia, wadada walishinda SAUT na wakaka akashinda Enock (katibu mstaafu) kutoka Bugando, mashindano ya kunywa soda mkaka alitoka Bugando wakati mdada alitoka SAUT.


     Matokeo ya pamoja, kutokana na pointi nyingi, Bugando walitangazwa kuwa washindi wa jumla .

       Picha na maelezo zaidi kutoka kwa dada ADELINA ALFRED aliekuwa mmoja wa waratibu wa bonanza la siku hiyo.

                               
                 .......wapendwa, tukumbuke michezo inaleta ushirikiano mwema, afya njema, pia ni furaha.
      
            .....Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja....     .      (Zab 133)..

             ........MUNGU WA MBINGUNI AWABARIKI WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA BONANZA HILO....AMEN..........
                           

      ............picha na matukio chini.........


   
 .....wenyeviti wa SAUT na Bugando wakishuhudia yanayojiri uwanjani....
 .....wanavyuo wakitazama michezo......
 ....wenyeviti wasaidizi wa matawi ya Bugando na SAUT wakijipanga kushindana mbio za mita mia....
 ....vijana wakisubiri kipenga kiwaruhusu wafanye yao katika mbio za mita mia...
 ...nao wadada hawakua nyuma katika mbio hizo....
 ....dada Frola kutoka Bugando akiibuka mshindi wa mbio za mita mia....

 .....mmoja wa waratibu kutoka Bugando Dr. Ben akitoa maelekezo.....
 .....vijana wakiwa mchezoni.....
 ...timu ya Bugando mpira wa miguu wakijiandaa kuingia uwanjani...
 ...dada Adelina (mratibu) akiwa na wenzake wakitazama yanayojili....
 ........ama kweli michezo ni furaha..nadhani unajionea mwenyewe...

 ...vijana wakionesha uwezo katika kasi ya kunywa soda kwa haraka zaidi....
 .......hata sisi wadada tunaweza kunywa....tushindwe tuna nini...?
 ...watazamaji....
 ....wakaka wakipimana nguvu kwa kuvuta kamba....
....wadada wakipimana nguvu ....
 ........mashabiki wengine nao walivutiwa na mashindano.....
 ......mwenyekiti na makamu (Bugando) wakifurahia ushindi wa kufukuza kuku .....
 .....mama Dafres nae akisherekea.......

No comments: