IBADA YA KUSIMIKWA VIONGOZI WAPYA WA USCF TAWI LA BUGANDO, (14/12/2014)


  •           Ibada ilifanyika katika ukumbi wa ( MD1 lecture hall), siku ya jumapili kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 4:30 asubuhi.








  •           Pia katika ibada hiyo, ripoti ya mapato na matumizi ya mwaka 2013/2014 ilisomwa na muhazini wa USCF wa mwaka 2013/2014 Mama Dafres.   

  •           Baraza la viongozi wa USCF mwaka  2013/2014 lilivunjwa rasmi na kuvishwa mataji, na baraza jipya la uongozi wa USCF 2014/2015 lilisimikwa rasmi na mtumishi wa MUNGU Mch. Kaene.



  •           Paradiso kwaya pamoja na timu ya kusifu na kuabudu walihudumu vyema katika ibada hiyo, na kubwa zaidi waliimba wimbo maalum kwa ajili ya kuwatakia washarika wote HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA WA 2015.


  •           Uongozi huo mpya uliweza kuanza na baraka za pekee, kwani siku ya kusimikwa kwao, wana USCF kwa pamoja waliweza kuchangia huduma ya kumuwezesha mtumishi wa MUNGU aliehudumu siku hiyo kupeleka injili katika kisiwa cha Kome.


  •            Mchana wa siku hiyo, saa 8:00 hadi 12:00, viongozi wapya waliweza kupata neema ya kuwa na semina ya NENOla MUNGU kuhusiana na uongozi.


  •            Hakika MWENYEZI MUNGU ni wa UPENDO na UAMINIFU kwani BARAKA zake zatutosha, tusichoke kumtafuta maadam anapatikana.




            TAFAKARI YA LEO; BWANA YESU ANATUFUNDISHA JINSI YA                                                                   KUTOA MAJIBU, JE MATENDO YAKO NI MAJIBU SAHIHI KWA JAMII INAYOKUZUNGUKA NA MBELE ZA MUNGU ?
                       SOMO; LUKA 7;11-23 

   

No comments: