........TAKE A TIME...

.......chukua mda, tafakari yote uliyoyaona, uliyoyasikia, uliyofanyiwa,uliyofanya, yaliyokukera,uliyoyazalau,uliyoyapenda,yaliyokufurahisha,.......


.....fikiri kwa mwaka mzima, umewaudhi wangapi, lakini umewasamehe wangapi, umeongeza marafiki wangapi,umepunguza wangapi, umesaidia wangapi nakadharika.....

......TAFAKARI UKUU WA MUNGU, KAKUSAMEHE,KAKUPENDA, HAKUKUACHA,KAKUVUSHA,KAKUFANYIA MAMBO MENGI USIOTEGEMEA....KA UKIJUA NI UPENDO WAKE NA NEEMA TUU...NA WALA SIO UWEZO,MATENDO AU AKILI ZETU.......

.........HAKIKA KAMA SI MUNGU...NA USEME SASA.....

......MSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA YOTE ALIYOKUTENDEA KWA MWAKA MZIMA......

.......UKUU, UPENDO, NEEMA, REHEMA NA AMANI YAKE IKUTAWALE MWAKA UJAO 2015.....


........nakutakia heri ya mwaka 2015....tembea na YESU...




....i wish u a happy new year in advance......

...may ALMIGHT GOD be with you throughout the coming year 2015....

...HERI YA KRISIMAS....

.......maana kwa ajili yenu (yetu) mtoto amezaliwa.
tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa
kifalme utakuwa begani mwake; 
naye ataitwa jina lake,
mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele.
Mfalme wa amani.

HERI YA KRISIMAS WAPENDWA

.......IBADANI LEO MJINI BUKOBA..

.....Ahsante MUNGU, nmeweza kushiriki katika Ibada ya Krisimasi katika usharika wa KKKT- Kanisa kuu Jimbo la Bukoba mjini.....

....Hakika MUNGU ni MWEMA na amezaliwa upya ndani ya maisha yagu....

...wewe je...?









......BEAUTIFUL SEASON OF THIS CHRISTMAS...

...may the blessings of Christmas be with you today and always...




...The gift of love.
The gift of peace.
The gift of happiness.
May all these be yours at Christmas......


... As you relish the goodies, decorate every nook and corner of your home and enjoy the get-togethers...
...May the joy and festivities continue to radiate in your lives,
long after Christmas is gone.
...Merry Christmas!....


...May all the sweet magic of Christmas conspire to gladden your heart and fill every desire...



WISHING YOU THE BEAUTIFUL SEASON OF CHRISTMAS !







.....WISHING YOU A MERRY CHRISTMAS....

.....Today in the town of David a Savior has been born to you: he is Christ the Lord......
                                                 ....Luke 2;11......


.....we have seen His star in the East, and have come to worship Him.......
                                              ......Mathew 2;2......

.....For unto us a child is born......
....Isaiah 9;6......

.....She shall bring forth a son, and thou shall call His name Jesus; for He shall save His people from their sins.
.....Matthew 1;21.....

........" Behold...
I bring you good tidings of great joy."...
.....Luke 2;11.....

.....The song of the Angels;
"Glory to God in the highest and on earth, Peace,"....
.....Luke 2;14....


...WAPENDWA TUSHIRIKI WOTE BARAKA HIZI....

....SHALOM ....

.......Kwaya ya USCF Bugando (Hautikisiki kwaya) wana tarajia kurekodi mkanda wa video (Video shooting) wa albamu yao inayojulikana kama, SEMA USINYAMAZE.Mkanda huo unatarajiwa kufanywa/ kurekodiwa mwezi wa tatu mwanzoni mwaka 2015.
.......Hivyo wewe kama ndugu, rafiki na mwenye mapenzi mema na Injili ya Bwana Wetu YESU KRISTO, unaombwa ushiriki wako wa hali na mali katika kutimiza jambo hili.

 .......Ushiriki wako waweza kua mchango wa mawazo, kipesa, pia na maombi ili jambo hili liweze kufanikiwa na kazi ya MUNGU isonge mbele.

........Kwa ushiriki wa jambo hili tafadhari wasiliana na ; 0757 086892- Mwenyekiti USCF
                                                                                       au;0783329500- Mwenyekiti Kwaya
                                                                                       au; 0767 964 793- M/msaidizi USCF
                                                                                        au; 0654132009 - blog admin

.........Pia ukihitaji fomu ya kuchangia, fomu zipo na utaratibu wa kukupatia upo. Kitu cha kufanya ni mawasiliano.

........UBARIKIWE NA KAZI YA MUNGU ISONGE MBELE........

.......KAZI YA BWANA TUITENDE KWA MOYO.....2 Wakorintho 4;1,  Matendo 8;21...........






.......THREE DAYS TO THE SPECIAL DAY.....

....3 days to christimas day.....
.....have you prepared your heart and mind to let HIM (JESUS CHRIST) to enter...?..
.......everything is ok..?
..........what about your neighbour who still don't know where he/she will get some food in Christimas day...

..............wish u the best preparations on that day....

........MERY CHRISTIMAS SERVANTS OF THE ALMIGHT GOD......


.....SHUKRANI KWENU WAPENDWA....

.....SHALOM,    
.....kazi yenu ni njema sana watumishi wa MUNGU, inatia moyo kuona blog hii inatembelewa na watu wengi kwa siku. Ukweli hali hii inafariji na kutia moyo sana. MBARIKIWE KWA HILO.

......ombi langu kubwa ni kuomba ushauri wenu kupitia comments au kuwasiliana na mimi moja kwa moja, mfano, je, muonekano wa blog hii kwenye simu ni mzuri, mbaya au turekebishe nini, na pia kupitia compyuta unaonekanaje.......
......je, vitu gani viongezwe au vipunguzwe au kurekebishwa na jambo lolote utakalojisikia....


.....wasiliana nami kupitia comments au no. 0654132009, au facebook (Samwel A Samwel), au whatsapp 0654132009.....

........nizidi kuwatakia maandalizi mema ya krisimas....

UJUMBE: ....'...Maandalio ya moyo Ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana....
                                                   
                                                Mithali 16; 1


....hepi holideiz wapendwa......

   

SI BUREEEEEEEE......NI KWA NEEMA TUUUUU............

......Shalom wapendwa......
.....ni furaha kubwa kuona tunaelekea mwisho wa mwaka 2014 tukiwa wazima, na wenye afya njema,...., lakini pia tukumbuke sio wote walomaliza mwaka, zipo tabu tulizopitia, wengine wametangulia mbele za haki na wengine wapo katika hali mbaya............basi tuungane kwa pamoja kumshukuru MWENYEZI MUNGU kwa yote yaliyo tokea kwa mwaka 2014, na pia awakumbuke wengine wasio katika hali nzuri.
....Pia nipende kuwatakia safari njema  wote wanaosafiri, watakao safiri  na waliokwisha safiri kuelekea sehemu mbalimbali, BABA YETU ALIYE MWAMINIFU ASIWAPUNGUKIE KWA JAMBO LOLOTE....AMEN...

JE, WAJUA YALIYOJIRI KATIKA BONANZA.......?

       Mnamo tarehe 13/12/2014 katika viwanja vya seminari vinavyopatikana ndani ya chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), kulikuwa na bonanza lililohusisha wanafunzi wa chuo kikuu cha kikatoriki cha Sayansi na Tiba Bugando na wale wa SAUT wote wakiwa ni kutoka kikundi cha USCF.

     Mashindano yalifunguliwa na mbio za wenyeviti, na Mwenyekiti wa Bugando aliwakilisha vyema kwa kuibuka mshindi wakati Mwenyekiti msaidizi wa SAUT nae aliibuka mshindi.

     SAUT waliweza kuibuka washindi katika mashindano ya kuijua vyema Biblia, mashindano ya kula, na kuvuta kamba.

     Wakati Bugando wakiibuka vinara katika mbio za mita mia, mbio za kupokezana vijiti,   kukimbiza kuku,pamoja na  kutembea na chupa kichwani

     Mchezo wa mpira wa miguu kwa wakaka, SAUT waliibuka washindi kwa kushinda goli tatu wakati Bugando wakishindwa kujitetea. (SAUT 3 - 1 Bugando).

    Mpira wa pete kwa wadada, SAUT walichakazwa na Bugando kwa magoli 13 kwa 1. (Bugando 13 - 1 SAUT).

    Lakini pia ipo michezo ambayo ilibidi pointi zigawanywe kwa wote, ambapo kukimbia kwenye magunia, wadada walishinda SAUT na wakaka akashinda Enock (katibu mstaafu) kutoka Bugando, mashindano ya kunywa soda mkaka alitoka Bugando wakati mdada alitoka SAUT.


     Matokeo ya pamoja, kutokana na pointi nyingi, Bugando walitangazwa kuwa washindi wa jumla .

       Picha na maelezo zaidi kutoka kwa dada ADELINA ALFRED aliekuwa mmoja wa waratibu wa bonanza la siku hiyo.

                               
                 .......wapendwa, tukumbuke michezo inaleta ushirikiano mwema, afya njema, pia ni furaha.
      
            .....Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja....     .      (Zab 133)..

             ........MUNGU WA MBINGUNI AWABARIKI WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA BONANZA HILO....AMEN..........
                           

      ............picha na matukio chini.........


   
 .....wenyeviti wa SAUT na Bugando wakishuhudia yanayojiri uwanjani....
 .....wanavyuo wakitazama michezo......
 ....wenyeviti wasaidizi wa matawi ya Bugando na SAUT wakijipanga kushindana mbio za mita mia....
 ....vijana wakisubiri kipenga kiwaruhusu wafanye yao katika mbio za mita mia...
 ...nao wadada hawakua nyuma katika mbio hizo....
 ....dada Frola kutoka Bugando akiibuka mshindi wa mbio za mita mia....

 .....mmoja wa waratibu kutoka Bugando Dr. Ben akitoa maelekezo.....
 .....vijana wakiwa mchezoni.....
 ...timu ya Bugando mpira wa miguu wakijiandaa kuingia uwanjani...
 ...dada Adelina (mratibu) akiwa na wenzake wakitazama yanayojili....
 ........ama kweli michezo ni furaha..nadhani unajionea mwenyewe...

 ...vijana wakionesha uwezo katika kasi ya kunywa soda kwa haraka zaidi....
 .......hata sisi wadada tunaweza kunywa....tushindwe tuna nini...?
 ...watazamaji....
 ....wakaka wakipimana nguvu kwa kuvuta kamba....
....wadada wakipimana nguvu ....
 ........mashabiki wengine nao walivutiwa na mashindano.....
 ......mwenyekiti na makamu (Bugando) wakifurahia ushindi wa kufukuza kuku .....
 .....mama Dafres nae akisherekea.......
IBADA YA KUSIMIKWA VIONGOZI WAPYA WA USCF TAWI LA BUGANDO, (14/12/2014)


  •           Ibada ilifanyika katika ukumbi wa ( MD1 lecture hall), siku ya jumapili kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 4:30 asubuhi.








  •           Pia katika ibada hiyo, ripoti ya mapato na matumizi ya mwaka 2013/2014 ilisomwa na muhazini wa USCF wa mwaka 2013/2014 Mama Dafres.   

  •           Baraza la viongozi wa USCF mwaka  2013/2014 lilivunjwa rasmi na kuvishwa mataji, na baraza jipya la uongozi wa USCF 2014/2015 lilisimikwa rasmi na mtumishi wa MUNGU Mch. Kaene.



  •           Paradiso kwaya pamoja na timu ya kusifu na kuabudu walihudumu vyema katika ibada hiyo, na kubwa zaidi waliimba wimbo maalum kwa ajili ya kuwatakia washarika wote HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA WA 2015.


  •           Uongozi huo mpya uliweza kuanza na baraka za pekee, kwani siku ya kusimikwa kwao, wana USCF kwa pamoja waliweza kuchangia huduma ya kumuwezesha mtumishi wa MUNGU aliehudumu siku hiyo kupeleka injili katika kisiwa cha Kome.


  •            Mchana wa siku hiyo, saa 8:00 hadi 12:00, viongozi wapya waliweza kupata neema ya kuwa na semina ya NENOla MUNGU kuhusiana na uongozi.


  •            Hakika MWENYEZI MUNGU ni wa UPENDO na UAMINIFU kwani BARAKA zake zatutosha, tusichoke kumtafuta maadam anapatikana.




            TAFAKARI YA LEO; BWANA YESU ANATUFUNDISHA JINSI YA                                                                   KUTOA MAJIBU, JE MATENDO YAKO NI MAJIBU SAHIHI KWA JAMII INAYOKUZUNGUKA NA MBELE ZA MUNGU ?
                       SOMO; LUKA 7;11-23