WORSHIP EXPLOSION LIVE CONCERT 2015- BUGANDO

""hakika ni jambo la kupendeza kukaa uweponi mwa BWANA MUNGU''''......

""uweponi mwake mimi natamani nikae daima nikitafakari Uzuri wake""......

..ndivyo ilivyokuwa katika tamasha la kusifu na kuabudu Bugando   ( Worship explosion Live Concert 2015)..


...tamasha lilifanyika siku ya Jumamosi tarehe 5 Disemba 2015 katika ukumbi wa Md 1......


... timu ya kusifu na kuabudu, kwaya, Paradise team, na waimbaji wengine wengi waliobarikiwa warishiriki tamasha hili...


............baadhi ya picha na matukio katika tamasha hilo...














HAKIKA BWANA WETU YESU KRISTO AWE NANYI WAANDAAJI WA TAMASHA HILI NA TUNATAMANI TAMASHA ZAIDI YA HILI WAKATI MWINGINE....


...baraka za Bwana zikae nanyi wote mlioshiriki kwa namna moja ama nyingine....


NB: KAMA ULIKOSA HILI!!!!!! BASI JIPANGE USIKOSE LIJALO.... 

SHEREHE YA KUWAKARIBISHA MWAKA WA KWANZA BUGANDO

tarehe 22/11/2015 ilifanyika sherehe ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza katika chuo Kikuu cha Bugando jijini Mwanza ikihusisha tawi la USCF.

Hakika watu walimuona Mungu katika sherehe hiyo, kwani mwaka wa kwanza walikaribishwa kwa namna ya tofauti sana na ilivyozoeleka.

Mchungaji James Kalekwa na walezi wa kikundi cha kikristo cha USCF nao warishirikiana na wana USCF katika sherehe hiyo.

Shukrani za pekee zimwendee Mwenyezi Mungu Baba wa milele aliyewezesha siku hiyo, walezi wa USCF, Mchungaji James Kalekwa na familia yake, Viongozi na wanachama wote wa USCF, na mwaka wa kwanza wote kwa ushiriki wenu.

baadhi ya matukio ya sherehe hiyo...












MUNGU AWABARIKI.


KARIBU MWAKA MPYA WA MASOMO 2015/2016

Ashukuriwe MUNGU wetu aliye juu aliye tuwezesha kumaliza likizo yetu tukiwa salama. Ikumbukwe wapo wenzetu waliotangulia mbele ya haki, tukimkumbuka mpendwa wetu DADA FRIDA aliyetutoka mwezi wa kumi mwaka huu...hakika tunaiombea roho yake ipumzike kwa amani pia tukiiombea faraja familia yake kwa ujumla.

Pia ukiwa mwaka mpya wa masomo 2015/2016, tumebahatika kupata wapendwa wengine wa mwaka wa kwanza kwa ngazi ya chuo, hakika karibuni sana CUHAS karibuni sana USCF.

Mwisho, tunaombwa katika mwaka huu wa masomo tuweke mipango yetu vyema ya kimasomo kadhalika na kihuduma. Tutembee na Mungu kila wakati na kila mahali maana tukimkaribia naye atatukaribia...tukimpenda naye antupenda zaidi. 
YEREMIA 1: 8-10
TUBARIKIWE NA MUNGU ALIYE HAI

JE UNAJUA NJIA YAJEHANAMU ILIVYO?


Ufunuo Wa Yohana 21:27

Watoto wa MUNGU nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI ambaye lengo lake yeye kuja ulimwenguni ni kututoa katika njia ya jehanamu na tumfuate yeye katika njia ya mbinguni. Nitaelezea kuhusu njia ya jehanamu uijue nitaelezea kimwili pia na kiroho. Njia hii ya jehanamu kiongozi wake ni yesu kristo wa uongo anaitwa wa uongo sababu ili amteke mtu silaha yake kubwa ni kumpa mwanadamu elimu ya uongo kwa kulibadilisha neno la MUNGU, na kuvunja amri za MUNGU.

1.     KIMWILI

Njia hii ya jehanamu kwanza kabisa ni pale unapoona mtu anatenda dhambi, anapoyatenda hayo yafuatayo nitaelezea haijalishi ameokoka au yeye ni mkristo hewa.
Kufanya uzinzi, ulevi, kuabudu sanamu, kuwa na wivu, chuki, kuvuta bhangi, sigara, madawa ya kulevya, kwenda disko, kucheza na kuimbe miziki ya kidunia, kusema uongo, kuoa wake zaidi ya mmoja, uwizi na matendo yote ya ufisadi (endapo unayefanya hayo uelewe upo katika njia ya jehanamu siyo ya mbinguni haijalishi unasema unaenda mbinguni) je hayo unayofanya ni matendo ya mbinguni? Jibu siyo.

2.     KIROHO

Haya nitakayoyataja ni baadhi tu ambayo yatakupa picha ujielewe katika roho je upo salama au tayari kiroho upo jehanamu na umeishikilia njia yake kwenda motoni. Kwanza kabisa hakikisha kuhani wako ni kweli MUNGU ndiye kamleta, kama amejiita au ni mchungaji wa mshara uelewe roho zenu zinapelekwa katika njia pana ya jehanamu katika ulimwengu wa roho , kuabudu sanamu, misalaba, ibada za wafu, ubatizo wa kikombe, maji ya kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji, kubatizwa ukiwa mtoto mdogo, kushiriki katika kanisa lolote lile ambalo linachangisha pesa kanisani au mahali popote pale, imeandikwa nyumba ya MUNGU ni nyumba ya sala, sasa ikiwa ni kinyume elewa hapo siyo mahali pa njia ya mbinguni, hapo ni mahali pa njia ya jehanamu katika ulimwengu wa roho, na uelewe pia ili uende mbinguni ni lazima katika uliwmengu wa roho uyafuate yale ya kweli tu katika biblia na siyo kinyume au kuchanganya uongo na ukweli hapana.

Kanisa lenye huduma sita zadala ya zile tano tu alizozianzisha YESU hapo pana njia ya jehanamu, huduma hii ya sita inaitwa Askofu, ukiona kiongozi wa kanisa amevaa kofia akihubiri ujue anawapeleka watu katika njia ya jehanamu. Zaidi soma makala ya Nabii Hebron Tanzania, nimeelezea mengi alivyonifundisha YESU ili niwafungue watoto wake macho na fahamu zao wapone roho zao sababu wengi mno wanapotezwa badala ya kuwekwa katika njia ya mbinguni sasa katika ulimwengu wa roho wameishika njia ya jehanamu. Japo na waumini hawapendi kwenda jehanamu, wanaongozwa na viongozi vipofu kiroho na kuwafanya waumini nao wawe vipofu wasimuone MUNGU wala kufika mbinguni. Ukiongozwa na mtumishi yeyote ambaye jina lake lipo kwenye mtandao wa freemason Internet au ni mchawi au mfanya mazingaumbwe, mfufua misukule au yeye mwenyewe hajabatizwa ubatizo ulioko katika katiba ya MUNGU yaani biblia, au anayeongozwa na nguvu za mizimu au anayejiita yeye ni YESU au kujifananisha na MUNGU au anajiita mungu mtu au mzinzi, mlevi, anachangisha watu pesa, hawa wote wanawapeleka watu jehanamu hayo ni matendo ya shetani na biblia imekataa. Au mtumishi yeyote aliyeitwa na YESU halafu akamsaliti hapo elewa hakuna tena njia ya mbinguni, ndani yake ni yesu wa uongo amekaa hivyo yesu huyo wa uongo atawaongoza watu katika elimu ya uongo ili awadumaze roho zenu na mpofuke msione njia ya mbinguni bali mbakie katika njia ya jehanamu na ile siku ya mwisho watu watalia na kusaga meno sababu watavuna wasichotegemea badala ya paradise ni jehanamu.

Mwana wa MUNGU ulilopo katika taifa lolote simama imara leo hii hali ni mbaya huu ni wakati wa hatari, kufumba macho na kufumbua ipo siku utakuta wengine wamenyakuliwa katika unyakuo na wengine walio katika njia ya jehanamu kimwili na kiroho watabakia hapo hapo wateseke kwa muda wa miaka saba na mpinga kristo, kataa sasa mafundisho ya mpinga kristo ili usije ukabakia hapa ulimwenguni wakati wa unyakuo, watakaobakia ni wale wapinga kristo (changanya neno na uongo) na watenda dhambi, na kila mtu ambaye hajaokoka na kuzaliwa mara ya pili. Zaidi uwatumie na wengine ujumbe huu ili wasome na wafunguke na wewe utabarikiwa na YESU WA NAZARETI.

NOTE:

BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote naomba leo uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele unitoe katika kitabu cha njia ya jehanamu, uniongoze wewe YESU na ROHO MTAKATIFU peke yake nyie ndio kweli, shetani sikutaki na mpinga kristo sikutaki katika jina la YESU WA NAZARETI aliye hai.

NABII HEBRON.

NOTE: IMENAKILIWA SEHEMU.

..TANGAZO..

........ANAYEHITAJI PICHA ZAKE ZA MAHAFALI YA USCF-BUGANDO, WASILIANA NA NAMBA YA SIMU 0654-132 009...ATAKUPATIA UTARATIBU WA KUZIPATA...

...PICHA ZIPO MFUMO WA (SOFT COPY)...

...MBARIKIWE NA SAMAHANI KWA KUCHELEWESHA.....





..BAADHI YA PICHA KATIKA MAHAFALI YA USCF-BUGANDO 2015...



....TUNAOMBA RADHI...

...idara ya mawasiliano na teknolojia ya USCF_BUGANDO, inaomba radhi kwa kutokua hewani kwa muda mrefu sasa...
..hii ni kutokana na baadhi ya changamoto zilizoikabili kwa kipindi hicho..

...Tuzidi kuombeana na kutiana nguvu ili kazi ya Mungu isonge mbele....

..AHSANTE MWENYEZI MUNGU...

....hakika tunayosababu na kusudi la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipindi chote hiki cha mitihani ya kumaliza muhula(semista ya 2,4,6,8,10) pia na  wengine wakiwa wanahitimu masomo yao moja kwa moja katika chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Bugando na BMC kwa ujumla...

...Pia shukurani zetu za dhati ziwafikie wahitimu wote, tumeuona mchango wao na kujitoa kwao katika kumtumikia Mungu na USCF kwa ujumla..Mbarikiwe...

...Bila kuwasahau Viongozi na wanaUSCF wote kwa ujumla, hakika kazi yenu sio bure....

..Tusisahau kuwaombea mwaka wa kwanza wanaofika vyuoni, ili kila mtu akakamilishe kusudi alilolibeba katika kanisa la Mungu na chuo husika...

...Mwisho, tuzidi kuifanya kazi ya Mungu huko tulipo, tusichoke....

BADO SIKU TATU TU...

BADO SIKU TATU ILI TAMASHA LA UZINDUZI WA MKANDA WA VIDEO WA NYIMBO ZA INJILI WA KWAYA YA USCF BUGANDO ( WANAHAUTIKISIKI) KUFANYIKA...

NI SIKU YA JUMAPILI TAREHE 21 MWEZI HUU(6) MAKA 2015 KATIKA VIWANJA VYA BUGANDO(BMC) ENEO LA LANGO KUU LA KUIMGILIA HOSPITAL YA RUFAA BUGANDO...

ITAANZA IBADA ASUBUHI KUANZIA SAA 1:30 ASUBUHI HADI SAA 4 ASUBUHI NA NDANI YA UKUMBI WA MD 1 HAPO CHUONI BUGANDO NA KUFUATIWA NA TAMASHA HILO KUANZIA SAA SABA MCHANA....

KWAYA, WAIMBAJI BINAFSI NA BENDI MBALIMBALI ZITAHUDUMU SIKU HIYO..

FIKA BILA KUKOSA NA USIKUBALI KUHADITHIWA PIA USIACHE KUCHUKUA CD YAKO MPYAAAAAAA KABISA NA MUNGU ATAKUBARIKI..

NB: MAOMBI YAKO  NI MUHIMU SANA



TAMASHA LA UZINDUZI WA MKANDA WA VIDEO YA SEMA USINYAMAZE

UMOJA WA KIKRISTO WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TANZANIA
(UNIVERSITY STUDENTS' CHRISTIAN FELLOWSHIP -USCF) 
                    WA CHUO KIKUU CHA BUGANDO                 


UNAYOFURAHA KUBWA SANA KUKUKARIBISHA/KUWAKARIBISHA WATU WOTE KATIKA TAMASHA LA UZINDUZI WA MKANDA MPYA WA VIDEO UNAOJULIKANA KWA JINA LA                                                                                    "SEMA USINYAMAZE".


TAMASHA HILO LITAFANYIKA SIKU YA JUMAPILI, TAREHE 21/06/2015 
KUANZIA SAA SABA MCHANA (7 MCHANA) HADI SAA KUMI NA MBILI JIONI (12 JIONI)
KATIKA VIWANJA VYA BMC ( LANGO KUU LA KUINGIA HOSPITALINI-BUGANDO)

MCHANGO WAKO NI MUHIMU LAKINI PIA KUFIKA KWAKO NI MUHIMU ZAIDI

PIA HAKIKISHA UNAPATA NAKALA YAKO ILI UKAONE VIJANA HAWA WANAVYOTUMIWA NA MUNGU....

NYIMBO KAMA UNIREHEMU, SEMA, WAKATI NA NYINGINE NYINGI ZIKIONESHWA LIVE BILA CHENGA..

UTAKOSAJE....MWAMBIE NA MWENZAKO KUHUSU TAMASHA HILI NA UTABARIKIWA..


mawasiliano: m/kiti kwaya -0759 329 500 / 0783 329 500
                   m/kiti kamati ya uzindizi-0655888581   























  ..HIZO NI BAADHI TU YA PICHA ZA VIJANA WAKIWA KAZINI