KARIBU MWAKA MPYA WA MASOMO 2015/2016

Ashukuriwe MUNGU wetu aliye juu aliye tuwezesha kumaliza likizo yetu tukiwa salama. Ikumbukwe wapo wenzetu waliotangulia mbele ya haki, tukimkumbuka mpendwa wetu DADA FRIDA aliyetutoka mwezi wa kumi mwaka huu...hakika tunaiombea roho yake ipumzike kwa amani pia tukiiombea faraja familia yake kwa ujumla.

Pia ukiwa mwaka mpya wa masomo 2015/2016, tumebahatika kupata wapendwa wengine wa mwaka wa kwanza kwa ngazi ya chuo, hakika karibuni sana CUHAS karibuni sana USCF.

Mwisho, tunaombwa katika mwaka huu wa masomo tuweke mipango yetu vyema ya kimasomo kadhalika na kihuduma. Tutembee na Mungu kila wakati na kila mahali maana tukimkaribia naye atatukaribia...tukimpenda naye antupenda zaidi. 
YEREMIA 1: 8-10
TUBARIKIWE NA MUNGU ALIYE HAI

No comments: