Ibada hiyo iliongozwa na kusimamiwa na wana-uscf kutoka Bugando...
utaratibu wa riturugia ukurasa wa sita na kuendelea......
kiongozi wa ibada alikua kaka :LUGINIO ILOMO
Mhubiri alikua mratibu wa maombi kaka: SHADRACK MWAKYELU
Wazee wa kanisa walikua ni watumishi wa MUNGU
- Emmanuel
- Vallelian
Somo la kwanza Ayubu 28:1-28
Somo la pili 1wakorintho 6:19-23
Mahubiri;
- MUNGU ni NURU wala giza halimo ndani yake...
- Giza ni matendo yote ambayo hayampi MUNGU utukufu
- MUNGU hapendi michanganyo (leo upo kwake, kesho upo sehemu nyingine)
- Ni heri ukawa moto au baridi ijulikane
- Ukiwa vuguvugu atakutapika.....
- kumbuka jehanam ipo, kwa wale wanaotenda mambo yasiyompendeza MUNGU
Ibada hiyo iliambatana na changizo kwa ajili ya video-shooting ya kwaya inayotarajiwa kufanyika mnamo mwezi wa tatu mwaka huu..
TAFAKARI YA LEO: Je! ni jambo gani unalofanya linaloleta mchanganyo mbele za MUNGU?
UJUMBE : Kumbuka unaemwabudu ni MUNGU sio mwanadamu hata adanganywe. Siku zote tembea nuruni ili uweze kufika Mbinguni.......
.....asante kwa kutembelea blog hii (pia tunapatikana facebook tembelea na like uscf bugando)......
MUNGU akubariki..
No comments:
Post a Comment