TATHIMINI YA IBADA YA UMOJA WA VYUO UKWATA MWANZA-ILIYOFANYIKA BUGANDO TAREHE 26/JANUARI/2014. 

HALELUYA;  BWANA YESU ASIFIWE ,
Kwa mapenzi yake mola ibada hiyo ilikuwa ya kubarikiwa sana kwa wanaukwata na wakristo wengine wote walohudhuria. Matawi ya UKWATA yaliyohudhuria yalikuwa matano yaani BUGANDO,VETA,FISHERIES,MIPANGO-BWIRU na BUTIMBA. 
Pia ibada hiyo ilikuwa na kwaya zilizotoa mahubiri kwa njia ya nyimbo zenye kumsifu Mungu na kwaya hizo ni CCT KWAYA BUGANDO, BUTIMBA KWAYA, WISDOM BAND na JERUSALEM BAND.
Mchungaji SEVERINE KISENGE alihudhuria pia ibada hiyo na aliyewalisha neno la Mungu siku ya ibada hiyo alikuwa mtumishi wa Mungu Mwalimu JAKOBO alihubiri sana juu ya UMOJA na WOKOVU kwa kusema kuwa sote tu madhehebu mbalimbali lakini tunamtumikia YESU KRISTO PEKEE na si binadamu kwa hiyo tunapaswa kumtumikia kwa umoja pia tunapaswa kumtumikia YESU KRISTO kwa unyenyekevu zaidi na tunapaswa kuwa na wokovu, na masomo yalipatikana katika ZABURI 133:1 , MITHALI 18:1, 1WAKORITHO 1:10 -13 , MARKO 7:21 - 23 na YEREMIA 32:40

                                  Mtumishi wa bwana Mwalimu JAKOBO akihubiri neno la Mungu.


                                       JERUSALEM BAND WAKITOA BURUDANI.

                  WARATIBU MBALIMBALI WA UMOJA WA VYUO UKWATA MWANZA.

                                                                  JERUSALEM BAND.


                                  Mch. SEVERINE KISENGE akitoa maelekezo mbalimbali.


                 WENYEVITI WA VYUO MBALIMBALI WA MATAWI YA UKWATA.


                                         WANAKWAYA WA UKWATA - BUTIMBA



                                                                    BUTIMBA KWAYA

SHUGHULI ZA UKWATA BUGANDO ZAANZA RASMI BAADA YA MAPUMZIKO MAFUPI YA KRISMASI

HALELUYA, BWANA YESU ASIFIWE.

UKWATA BUGANDO tuna mshukuru sana Mungu kutulinda katika mapumziko mafupi ya krismasi na kuturudisha chuoni tukiwa salama na hivi tanatangaza kuanza shughuli za chama rasmi kuanzia tarehe 06/01/2014 vipindi vya katikati ya wiki asubuhi na jioni bila kusahau kwaya siku za wik end jioni. Tunaomba uungane nasi katika maombi kwa kipindi kinacho fuata chote kiwe na mafanikio katika mipango yote iliyopo ili watu wapate kumjua Mungu na kufanya mapenzi yake. Mungu akubariki kwa kuungana nasi.


Mwenyekiti wa UKWATA BUGANDO Ndg. Amos Brighton akitoa maelekezo na kufafanua matangazo mbalimbali na jinsi ya kuyakabili majukumu mbalimbali kwa mwaka 2014.

IBADA YA KUSIMIKA VIONGOZI WAPYA WA UKWATA TAREHE 08/12/2013.

HALELUYA, BWANA YESU ASIFIWE.
SHUKRANI ZI MFIKIEYE MWENYEZI MUNGU NA KILA ALIYE SHIRIKI KATIKA IBADA YA KUWASIMIKA VIONGOZI WAPYA WA UKWATA BUGANDO KWA KIPINDI CHA 2014/2015, IBADA ILIFANYIKA KATIKA DARASA LA MD1 , VIONGOZI WOTE WALIOKUWA WACHAGULIWA WALISIMIKWA NA MCH.MASAGA KUTOKA AICT - NYAKATO.

NENO LA MUNGU LIKIONGOZWA NA Mch.MASAGA,  SOMA Waefeso 4:17-25 , NDIYO UJUMBE TULIYO PATA KATIKA IBADA HIYO, Viongozi wote walisisitizwa kama maandiko yanenavyo wafanye kazi kwa bidii sana na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo na kuwa mfano na kielelezo kwa wakristo wote.

 Picha ya kwanza hapo chini. Mch.Masaga akimsimika Mwenyekiti wa mpya wa Ukwata Bugando,ndg.Amos Brighton.

Picha ya pili hapo chini .Wa kwanza kutoka kulia ni Mwenyekiti Amos Brighton, wa pili ni M/Kiti msaidizi Wokuheleza Buberwa, watatu Katibu wa ukwata Enock Sweya, wa nne Emanuel Mtaki mwakilishi MD2, wa tano Dafres Chirwa mweka hazina ukwata.                                                                                                                     

IBADA YA KWANZA YA VIONGOZI WAPYAWA UKWATA YA TAREHE 12/JANUARI/2014

    HALELUYA , BWANA YESU ASIFIWE SANA,
Shukrani na sifa zimfikie mwenyezi Mungu na kila mkristo aliyeshiriki ibada ya kwanza ya viongozi wapya wa UKWATA - BUGANDO na ibada ilikuwa yenye kupendeza na kila mmoja alibalikiwa kimwili na kiroho.
neno la Mungu liliongozwa na Mch.Kaene kutoka kanisa la Anglikani St.Nicholaus, soma Isaya 61:10 na Isaya 62:1-10 ndiyo ujumbe wa Mungu tuliolishwa siku ya ibada hiyo.



                 Wana Ukwata Bugando wakiwa katika ibada hiyo.

IBADA YA PAMOJA NA UZINDUZI WA ALBUM YA PILI YA KWAYA YA CCT TAREHE 16/FEBRUARI/2014.

                                  "BWANA YESU ASIFIWE SANA"
Wapendwa katika bwana kwa upole na hofu zaidi UKWATA-BUGANDO unawakaribisha wakristo wote kwenye ibada ya pamoja siku ya tarehe 16.02.2014 siku ya jumapili kuanzia saa 1:30-4:00 asubuhi katika darasa la MD1, ikifuatiwa na ibada ya uzinduzi wa album ya 2 ya audio kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 11:30 jioni ,uzinduzi utafanyika katika viwanja vya BMC,nyote mnakaribishwa mje mburudike na kubarikiwa kwa nyimbo nzuri sana kimwili na kiroho pia. Jina la album hiyo ni "SEMA USINYAMAZE"





                                                                            WANAKWAYA YA CCT UKWATA BUGANDO(HAUTIKISIKI)